Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na
mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili
wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni
Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa
jina la Papii Kocha).
Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote
zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na
zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na
wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu
wa Sheria.
Jeshi la
Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na
linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza
ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa
kisheria.
Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa
kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo
vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria
uchukue nafasi yake.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014
No comments:
Post a Comment