STORY
BARAKA R. LAZIMA
TITTLE
SITALIA TENA
Danieli ni kijana aliekuwa msomi sana
kakiri kutokana na ugumu wa maisha alijikuta kaingia kwenye matatizo makubwa
sana, na kujikuta kapoteza dira ya maisha yake.
Hakujua la kufanya kujikuta akitoa machozi bila kikomo lakini alitafuta
mbinu ya kujifuta machozi yaani alitoa kauli moja (sitalia tena je, alikuwa na
maana gani basi fuatilia tamthilia hii ya kusikitisha sana na kusisimua sana
sitalia tena.
Sehemu ya kwanza (1)
Daniel alikuwa kwenye gari la kifahari sana
alikuwa mwenye mawazo sana lakini alikuwa na hamu sana ya kuona familia
yake. Akiwa anakaribia kufika nyumbani
kwao alkuta mji apo kimya sana lakini alishangaa sana akiona mazingira
yamebadilika sana, ulikuwa ni muda mrefu sana tangu aondoke nyumbani kwao.
Daniel akiwa anakaribia kufika nyumbani
kwao alishangaa sana kuona anawaona watu wamejaa kwao, alishuka kwenye gari ili
aone kunanini aliposhuka kwenye gari watu wengi walimwangalia kwa mshangao sana
wengine walimuogopa sana lakini baadhi ya watu walimzuia asiingie ndani watu
walio ndani walishangaa kusikia kelele walitoka nje, Daniel alishangaa sana
kumwona binti mmoja ata yule binti alipomuona Daniel aliogopa sana na
alimkumbatia mama yake huku akilia akisema katika tukio la siku ile ambalo
tulitekwa na baadhi yetu waliuawa na wengine tulibakia basi mmoja wa watekaji
huyu alikuwepo yaani (Daniel). Machozi
yalimtoka mama yake binti. Jina lake
aliitwa Doreen ni mke wa Daniel na yule binti ni mtoto wa Daniel lakini muda
mrefu sana Daniel alikuwepo alimwacha mtoto wake akiwa mdogo sana miaka 5 na
saizi ana miaka 12. Daniel akiwa bado
anamshangaa yule binti huku akikumbuka kitendo alichomfanyia, Doreen akaenda
kwa hasira na kumzaba kibao Daniel, Daniel ni unyama gani umeufanya umefanya
mabaya mangapi ukaona haitoshi na ukaenda kumwiba binti yako, Daniel alishangaa
sana kusikia kauli hiyo, Daniel akamuuliza Doreen anasema huyu binti ni mtoto
wangu, Doreen akajibu ndio ni damu yako, Daniel akajikuta akitoa machozi na
kuomba msamaha akidai hana maisha tena, kwa unyama aliufanya akaomba msamaha
lakini yule binti alilia sana na akasema wewe sio baba yangu mimi sina baba,
Daniel yale maneno yalimuuma sana yakamfanya alie kwa uchungu huku watu
wakimshangaa. Pia Daniel alimwomba mke
wake amuitie mama yake amuombe msamaha, Doreen akamshangaa Daniel akamwambia
kweli wewe ni shetani ulie changanyikiwa ulifikiri umekuja baada ya kusikia
mama yako kafariki huoni umati wa hawa watu, Daniel hakuamini machoni mwake
kuambiwa maneno hayo, moyo wake ulimuuma sana na kujikuta anabubujikwa na
machozi alikuwa na maumivu makali moyoni mwake.
Daniel alimpenda sana mama yake alienda kutafuta maisha kwa ajili ya
familia yake hakuamini machoni mwake akiwa na mawazo kichwani mwake akaingia kwenye
gari akaendesha kwa kasi huku akinywa pombe kali kwa hasira yote hayo alowatamu
mtu mmoja. Alikuwa mwendo kasi akielekea
kumuongamiza mtu huyo. Lakini mawazo
yake akaona bora aende kituo kikuu cha polisi ili aonane na kamanda wa polisi
kwani alimuamini sana mtu huyo kwani Daniel alizijua sana siri nyingi za nchi.
Daniel akiwa anaelekea kituo cha polisi
lakini alijua kuwa anatafutwa kwa muda mrefu na polisi, akapata jibu jinsi ya
kuingia kituo cha polisi. Daniel alikuwa
na silaha kali kali sana liingia duka moja jirani na kuwataka baadhi ya watu na
kuwaagiza kwenye gari na kuwahinga pingu alikuwa na silaha nyingi sana
aliendesha gari kwa kasi sana wale matekwa walishangaa kumuona mtekaji
anaelekea kituo kikuu cha polisi, Daniel alipofika karibu na kituo cha polisi
alishangaa polisi wakiwa bize na magari yao huku wakiwasha king’ora basi yao
alipishana nao. Kumbe polisi walipigiwa
simu kuhusu watu waliotekwa lakini polisi hawakutambua lile gari kwani
hawakupewa taarifa kwa undani magari mengi yalimpita Daniel. Kituo cha polisi kilibakia na askari wachache
sana. Daniel alishuka kituo cha polisi
huku akiwashirlia wale mateka na akiwa ameshika mabomu mkononi na mashine kubwa
sana ambayo baadhi hata askari hawajawahi kuona atakusikia bunduki ile ombi la
Daniel lilikuwa moja akiwambia askari waliojificha
ndani ya kituo cha polisi huku wengine wakiwapigia simu akdari walioenda
kumtafuta mtekaji. Daniela aksema sina
ubaya na jeshi la polisi naomba nionane na kamanda wenu ndani ya dakika 5
msipofanya hivyo wale mateka atakuwa halali yangu pamoja na hiki kituo
chenu. Askari walikuwa hawajibu
wakamuomba mkuu wao aikilize maelezo ya Daniel, mkuu wa kamanda alikuwa mbali
kutokana na uzalendo wake na kuapa alichokula akuogopa kituo maisha yake kwa
ajili ya raia wake aliopewa dhamana na kuwalinda kwa mujibu wa katiba ya
muungano wa Tanzania, akatoka nje na
akiwa ameweka mikono juu na huku akijitambulisha kuwa yeye nide kamanda wa
polisi. Daniel alicheka kidogo kasha akatoa machozi akisema wewe tangulika
mbali sana ongera kwa kazi nzuri sana.
Kamanda wa polisi alishangaa sana kusikia
yule mtekaji anamjua vizuri, Daniel akajitambulisha jina lake pia akamuomba
kamanda najua unalijua sana jina hili ni mimi mwenyewe ulikuwa unanitafuta kwa
muda mrefu sana kamanda hakuamini machoni mwake na pia alishangaa sana. Na kumuuliza Daniel naomba uwaachie hao
watu. Daniel akajibu sina shida na hawa
watu naomba tuongee na wewe mimi si muhalifu tena nimekuja na mambo mengi sana
tafadhali niamini kamanda alimsikiliza kwa makini Daniel kasha akamsogelea
Daniel alikuwa na pingu mkononi akamshika kamanda akajifunga nae huku akisema
kwenye kiuno changu nimevaa mkanda wa bomu endapo vijana wako watafanya lolote
nitaacha fyuzi bomu litalipuka tutakufa wote, kamanda akatoa amri kwa vijana
wake wasifanye lolote. Daniel akamwambia
kamanda kuwa nina siri kubwa sana ila kabla ya yote naomba tuende nyumbani
mkamzike mama yangu baada ya hapo nitakuambia kila kitu. Kamanda akatoa amri baadhi ya vijana wake
waongozane. Daniel aliomba watumie gari
lake na pia katoa amri kuwa wote mateka waachiwe hana ugomvi nao bali ilikuwa
ni njia kuu ya kufika hapo kituo cha polisi.
Daniel akawaomba radhi na kusema poleni sana msiogopoe sina nina ya
kuwazuru mmenisaidia tu lengo langu la kuwateka nilitaka kuonana na huyu
mheshimiwa. Daniel akamfungua mlango wa
gari na kuwaamuru askari mmoja achukue kitita cha fedha awapatie wale mateka
kama kuwapotezea muda wale mateka hawakuamini kupewa fedha nyingi kiasi kile.
Daniel akiwa kajifunga pingu na kamanda wa polisi wakaingia kwenye gari na
kuelekea kwenye msiba wa mama yake huku askari akiwa anendesha gari. Walipofika nyumbani alimkuta watu wanafanyika
kutoka makaburini. Daniel aliumia sana.
Umati wa watu walishangaa sana kuona magari
ya polisi na kumuona kamanda wa polisi akiwa amejifunga pingu na Daniel. Daniel aliwafuata mke wake na kuomba
akamuonesha alipopumzika mama yake.
Daniel akamfungua pingu kamanda na akajifunga yeye na akamkabidhi huyu
kamanda na akamwambia kuwa yeye sio muhalifu tena amuamini maneno yake. Daniel akiwa chini ya ulinzi wakampeleka
makaburini. Daniel alioneshwa alipolala
mama yake. Daniel alilia kwa uchungu
sana na kumuahidi mama yake kuwa anatugokoa lakini sio muda atamfuata yeye
kuomba msamaha. Doreen aliongea kwa uchungu huku akimwambia Daniel kilio cha
mama yako kimesababishwa na wewe. Mama
yako alipata ugonjwa kiarusi baada ya kusikia unatafutwa na polisi huku vyombo
mbalimbali vya habari vikiandika jina lako unatafutwa, maneno yale yalimuuma
sana Daniel akamwambia mke wake achukue begi ndani ya gari lilikuwa na pesa
nyingi sana, kasha Daniel akmwambia mke wake leo itakuwa ndo mwisho wa kunana
kwani aendako ajui kama atakuwa salama alimkabidhi na hati mbalimbali za mali
zake na kumweleza mahali zilipo kasha Daniel akamuomba mkuu wa polisi ampeleke
kituo cha polisi akamweleze kila kitu na kumwambia anazo siri nyingi sana.
Daniel akamuaga mke wake huku akitokwa na
machozi wote kwa pamoja walilia sana.
Daniel akiwa chumba maalum cha polisi akiwa na wakuu wa kituo. Kamanda
akamuuliza Daniel tueleze kwanini ulifanya matukio makubwa namna hii na
kiongozi wako ni nani alikuwa anakutuma?
Daniel aliinama kichwa chini huku akitokwa machozi kasha kaaza kusimulia
mkasa wote tangu utotoni mwake. Fuatilia
kisa hiki ujue hatima ya Daniel.
MWENDEZO WA HII STORY
ReplyDeleteStori qaliiiii
ReplyDeleteSana zmezid mno,,,punguza nrno sana
ReplyDelete