Kufuatia kuripotiwa kwa habari "kali" sana iliyopewa kichwa "DIAMOND AFICHUA KISA CHA KULALA NA UWOYA!"
leo kuhusu mwanadada Irene uwoya na Msanii wa kizazi kipya Diamond
platnumz leo na mtandao wa Global publishers, hatimaye Irene Uwoya
alichukua dakika kadhaa kuandika hichi alichokiandika hapa chini....
“Kuna saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio
anageuka...kwanin ukiwa muwaz watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia
sanaaa kuliko skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki
yangu anaweza kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na
rafik wa kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me
better”
MCHUNGUZI wa mambo anasema maneno hayo ni
kutokana na kile alichokiona kama ni usaliti wa namna fulani toka kwa
rafiki yake wa karibu (Jina kapuni) kuamua kumuanika hadharani mdada
huyo wa bongo movies
Kama hukupata nafasi ya kuisona habari hiyo toka
kwenye mtandao wa global publishers basi isome hapa kama tulivyoinukuu
toka mtandao huo....
""SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni
mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
KISA KAMILI
Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa
ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa
kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili,
kilichomfanya Diamond kufikia hatua ya kumtongoza na kutoka naye
kimapenzi, ni kitendo cha Uwoya kutoa maneno ya kumponda huku akionesha
waziwazi hali ya kumchukia kila walipokutana.
UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND
“Unajua Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na
mara nyingi alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa
zikimfikia mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo
ndiyo zilichochea.
“Kufuatia hali hiyo, Diamond naye kila alipofikishiwa taarifa na
mashosti wa Uwoya, alikuwa akijisikia vibaya mno ndiyo maana ‘Sukari ya
Warembo’ alilazimika kumvizia Uwoya kwa hali na mali ili kumfanya
ampende.
CHIKOKA ATAJWA
“Nakumbuka kwa mara ya kwanza Diamond alimtuma (Juma) Chikoka ‘Chopa’ kwa Uwoya ili amfikishie ujumbe wa yeye kumtaka.
“Chikoka hakufikisha taarifa hizo, kitendo ambacho kilimuuma
sana lakini siku moja Diamond alikutana na Uwoya akiwa na Chikoka,
maeneo ya Sinza-Mori (Dar), akamuomba tena Chikoka namba, akampa, hapo
ndipo uhusiano ulipoanzia.
“Siku mbili baadaye Diamond alizungumza vizuri na Uwoya. GLOBAL NOMA “Diamond aliomba ahadi ya kukutana na mwigizaji huyo, bila kuchelewa, Uwoya aliiva na kukubali ambapo walikutana kwenye ile hoteli mliyoandika (Global) kule Mbezi Beach (Dar) wakamalizana. “Unajua Diamond alifanya hivyo kwa sababu ya kupondwa na washikaji zake kuwa anatamba kutembea na mastaa lakini hamuwezi Uwoya. “Kwa hiyo utagundua chanzo cha yote ni mdomo wa Uwoya kutangaza kutompenda Diamond kwani alikuwa akimsema vibaya sana kwa watu wake wa karibu,” kilidai chanzo chetu.

Chanzo:Bongomovies.
No comments:
Post a Comment