Mwanamke
ambaye pia ni DAKTARI wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Salha
Hassan amejikuta akipigwa talaka na mume wake, Abdullatif Mohamed
kufuatia picha zake chafu akiwa na mwanaume mwingine kunaswa kwenye simu
yake mkononi, Uwazi limenyetishiwa.
Cheti cha ndoa ya Salha Hassan na mume wake, Abdullatif Mohamed. |
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Abdul alisema alifunga ndoa na Salha Februari 15, 2007 na waliishi kwa upendo mkubwa.
Abdul alisema kuwa mwaka 2010 mkewe aliondoka Zanzibar na kwenda
kuongeza ujuzi kwenye Chuo Kikuu cha Udaktari Muhimbili jijini Dar es
Salaam.
“Akiwa pale Muhimbili mke wangu alinieleza kuwa simu yake ya mkononi
(Nokia) inamsumbua sana, nikamshauri kwamba akirudi huku tuiuze halafu
nimnunulie nyingine,” alisema Abdul.
Salha Hassan akiisaliti ndoa yake. |
Aliongeza
kuwa, katika mwaka wa tatu, mkewe alipofanya mtihani alifeli, hivyo
akalazimika kurejea Zanzibar kuendelea na kazi katika hospitali
anayofanyia kazi.
“Siku kadhaa baada ya kurejea, nilichukua simu yake kwa lengo la
kwenda kuiuza kama tulivyokubaliana, lakini mke wangu alitoa ‘memory
card’ yake ambayo najua mlikuwa na vikorokoro vyake, hilo
sikulifuatilia. “Tayari nilishapata mteja,
tukakubaliana bei lakini kabla ya kumkabidhi niliamua kufuta vitu
vingine ambavyo vilikuwa ndani ya simu ya mke wangu. Wewe mwandishi
unajua, simu zina ‘dokumenti’ mbalimbali,” alisema Abdul.
Abdul alisema kuwa akiwa katika zoezi la kufuta kumbukumbu
mbalimbali zilizokuwemo kwenye simu hiyo, ghafla alizibamba picha chafu
za mke wake akiwa na mwanaume mwingine ambaye hakumjua. “Nilishtuka
sana, sikuwahi kufikiria. Hata hivyo, awali nilidhani naota ndoto,
lakini baadaye nikajiridhisha kwamba sikuwa ndotoni,” alisema Abdul.
Mwanaume huyo aliongeza kwamba, kufuatia tukio hilo baya machoni mwake alijikuta akianguka na kupoteza fahamu.
Abdul alimuonesha paparazi wetu picha alizozinasa ambapo moja, Salha
anaonekana amelala kitandani akiwa amenyoosha miguu kwa kujisitiri na
‘kufuli’ tu. Picha nyingine amepozi kwa kuegemeana na mwanaume huyo
ambaye Abdul alisema anaamini anaishi jijini Dar es Salaam au alikuwa
akisoma naye Muhimbili. Picha nyingine, Salha anaonekana amepozi katika
mkao tata akiwa mtupu. Picha mbili zilionesha alijipiga mwenyewe
isipokuwa ile aliyolala kitandani.
Abdul alisema kuwa kufuatia kuuona uozo huo wa mke wake aliyempenda
sana, baada ya kuzinduka alibatilisha uamuzi wa kuiuza simu hiyo na
kurejea nyumbani ambapo alipomuuliza, mwanamke huyo hakuwa na majibu ya
kujitosheleza. Waligombana sana na mwishowe aliamua kumrudisha nyumbani
kwa wazazi wake ‘akimsindikizia’ talaka juu kwamba si mke wake tena.
Akasema: “Kwa kweli sikuweza kukivumilia kitendo kile, haikuwa nia
yangu kumpa talaka lakini moyo ulishindwa kuvumilia kuona mke wangu yupo
kama alivyozaliwa.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Salha kwa
njia ya simu yake ya kiganjani ambapo baada ya kumpata na kumsomea
mashitaka yake kuhusu picha hizo, alijibu kwa jeuri: “Mimi naona
ulizokuwa nazo (picha) hazikutoshi kabisa. Ninazo nyingine, kama upo
tayari nikutumie ili uziongezee kwenye habari yako. Kwanza mimi siyo
daktari. Uwazi: Sikia Salha… Salha akakata simu.
Uzoefu unaonesha kuwa, tangu simu za mkononi zilipoingia nchini
Tanzania, wapendanao, wakiwemo wachumba, wamekuwa wakiingia kwenye
migogoro mikubwa inayosababishwa na matumizi mabaya ya simu hizo. Ni
vyema wapendanao wakachukua tahadhari kuhusu matumizi ya simu zao.
Baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya ndoa wanasema kuwa hakuna kiwango
cha juu cha wanandoa kutopendana kama usaliti..
No comments:
Post a Comment