MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Sunday 14 September 2014

ONA JINSI SERENGETI FIESTA ILIVYOSAMBAZA KIFO SHINYANGA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMRAV6ujqUFdXZBlntO8NyWNf8LWBh1fI7gdpNhQNdkHBmSJWywWZphY8yWI_pkQHcb53tTCjBraxc-HozgIYvk4J96a0KjSgR53hiUeiZes44FwoDiA2Y4tUQ3v9J9X9Vv4HQbU6jVVZz/s640/FIESTER+1.jpg
Mwili wa marehemu Mussa ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakati wa kufanyiwa postmoterm leo



Mwili wa marehemu Mussa ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakati wa kufanyiwa postmoterm leo

Wakazi wa shinyanga wakijiachia kwenye tamasha hilo masaa machache kabla ya tukio.


Tamasha maarufu nchini hapa linaloratibiwa na kikundi cha Clouds media Group, chini ya udhamini wa kinywaji cha Serengeti maarufu kama “SERENGETI FIESTA” na mwaka huu Tamsha hilo likiwa na kauli mbiu yake iitwayo “SAMBAZA UPENDO” limeingia dosari baada ya kutokea mauaji wakati tamasha hilo likiendelea.
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mussa Shija (17)  mkazi wa kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga aliyeuawa kwa kupigwa kitu kizito kichwani na watu wasiofahamika akiwa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililokuwa linafanyika usiku wa kuamkia leo katika uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga
Akizungumza na Malunde1 blog mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema uchunguzi  wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mussa Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kijana huyo aliuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana nje ya fensi la uwanja mdogo wa Kambarage palipokuwa panafanyika tamasha la Fiesta.
Hata hivyo amesema jeshi la polisi litatoa taarifa kamili baadaye kwani linaendelea kufanya uchunguzi

No comments:

Post a Comment