MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday 12 March 2014

INASIKITISHA MAMA NA MWANA WAFA PAMOJA KWA AJARI, WAZIKWA MJINI IRINGA (MAKANYAGIO) SOMA ZAIDI

MAMA NA MWANA WAFA AJALINI IRINGA. WAZIKWA PAMOJA....

MIILI YA MAMA NA MTOTO IKIWA KWENYE MAJENEZA TAYARI KWA KUAGWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA IRINGA BAADA YA AJALI
IRINGA
FRANK KIBIKI
MUUGUZI wa hospitali ya mkoa wa Iringa, Rose Stambuli (56), na mwanae Daton Ilomo (23) ambaye ni mwanafunzi wa ICT katika chuo kikuu cha mlimani, wamefariki dunia baada ya gari aina ya Noah walilokuwa wakisafiria kupasuka taili, na kupinduka.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Igingilanyi, nje kidogo ya manispaa ya Iringa na kuacha simanzi kubwa kwa ndugu jamaa na marafiki, hususani mtoto pekee aliyebaki katika familia hiyo, Lusajo Mwakabuku.
Akisoma taarifa ya kifo hicho mara baada ya miili hiyo, kuagwa hospitali ya Mkoa, Mmoja wa madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Dk Yahaya Msigwa amesema, mama alifariki juzi jioni wakati mtoto akifariki leo.
Mama na mwanaye wote wamezikwa pamoja, katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa baada ya kufanyika ibada katika kanisa la RC la Mshindo.
Muuguzi huyo ambaye alikuwa na watoto wawili, amemuacha mtoto mmoja Lusajo Mwakabuku ambaye ni mwanahabari kitaaluma.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe.
Amina

No comments:

Post a Comment