HATIMAYE AJIRA MPYA ZA WALIMU KUTANGAZWA TAREHE 15, TAARIFA TOKA TAMISEMI HII HAPA
OFISI ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza ajira mpya za
walimu wapya 36,021 waliohitimu mafunzo ya uwalimu mwaka 2013.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TAMISEMI,
Jumanne Sagini alisema walimu hao wataajiriwa na mamlaka za Serikali za
Mitaa, Aprili mosi mwaka huu.
Alisema kati ya idadi hiyo, walimu wa
ngazi ya cheti (Daraja III A) ambao watafundisha shule za msingi ni
17,928 na walimu wa shule za sekondari 18,093 wakiwemo 5,416 wa
stashahada na 12,677 wenye shahada.
“Orodha rasmi ya walimu wapya
ambayo itaonesha halmashauri mbalimbali walizopangiwa walimu hao
itatangazwa kwenye tovuti ya TAMISEMI na ile ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Machi 15 mwaka huu,” alisema Sagini.
Aliongeza
kuwa, walimu hao wanatakiwa kuripoti kwenye halmashauri husika
walizopangiwa ifikapo Aprili mosi mwaka huu ili taarifa zao za
kiutumishi zifanyiwe kazi na waajiri wao ambao ni Wakurugenzi ili waweze
kupata mishahara yao.
“Upangaji walimu wapya kwenye halmashauri
umezingatia uwepo wa mahitaji ya walimu, fedha za kujikimu kwa muda wa
siku saba na nauli ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu ambaye ataripoti
kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali,” alisema.
Aliongeza
kuwa, TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kazi kwa walimu
wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho
credit by tamisemi website, habari hii ni ya kweli wala si uzushi waweza
kwenda kwenye website ya tamisemi kwa kubofya link hii hapa www.pmoralg.go.tz ,
bofya hapa kuona
No comments:
Post a Comment