MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Saturday 5 October 2013

IRINGA MOVIE WAPATA VIFAA VYA MICHEZO KUTOKA KWA MWAKALEBELA, HII IKIWA NI MOJA YA MIKAKATI YA KUINUA SANAAA MKOANI IRINGA

                                           timu ya Iringa Movie ikiwa katika picha ya pamoja

Hatimaye timu ya Iringa movie yapata vifaa vya michezo kutoka kwa moja kati ya wadau wake Ndugu MWAKALEBELA Hii ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya iringa movie na mafanikio pia ukitofautisha na mwanzo ilipoanzishwa. kiukweli tunaweza kusema ni kitu cha kujivunia kwa kuwa na mafanikio na tunazani kufikia siku za hivi karibuni tutakuwa tumepata mafanikio zaidi moja kati ya wadau alielezea hivyo

  baadhi ya wanachama waelezea changamoto wanazokutana nazo na wamedai hii ni kama njia ya mafanikio ya kundi hili ambalo linafanya vyema kwa sasa kwani limeweza kushiriki katika mafunzo ya sanaa kwa ujumla na nia ikiwa ni kuleta utofauti katika tasnia ya filamu mkoa wa Iringa ambao ukiuzungumzia kipindi cha nyuma ulikua ni mkoa ambao upo chini kidogo katika suala zima la filamu




                         moja ya wachezaji wa Iringa Movie wakiwa katika picha

                                              wacheza wakiwa katika picha ya pamoja

Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na F. Mwakalebela ni pamoja na jezi kwa wadada na mpila kama wanavyoonekana katika picha ya pamoja. Hii inaleta fulsa kwa wadau wengine wa filamu mkoa wa Iringa kujitokeza kuhakikisha mkoa unafanya vizuri zaidi katika sanaa kwa ujumla


Kwa wale walio Wilayani pia mnakaribishwa kujiunga na Iringa movie kwa kufika ama kuwasiliana na wahusika kwa kua fomu zipo kwa wale wanaohitaji kuwa wanachama hai wa Iringa Movie ni mapema wala ujachelewa . Hii ni kuakikisha wote tunashiriki bil kujali ulipo mnakaribishwa wote.




Shukrani za dhati kwa viongozi ambao wametumia muda wao kwa upendo wa kweli na mkoa wao (Iringa) kuakikisha inarudi katika ramani ya sanaa na kufanya vizuri zaidi pia wale wote walioonesha upendo wa dhati kushiriki/ kuwa wanachama ambao wanauchungu na sanaa na wanajua nini maana ya sanaa katika muendelezo wa mafanikio ya sanaa mjini iringa 


No comments:

Post a Comment