Bajeti ya Tanzania imelenga kuinua maisha ya wananchi wa vijijini hususan katika sekta ya Kilimo, Nishati na Maji huku ikiacha sekta ya Elimu ambayo ilileta msug
uano mkubwa hivi kariubu kati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na wadau wa walimu.
Wananchi pamoja na wadau wa elimu walitarajia kwamba majeti hiyo itatoa kipaumbele katika sekta ya elimu ilikupunguza idadi kubwa ya wanafunzi wanaofeli katika mitihani ya darasa la nne, la saba,kidato cha pili,kidato cha nne na hata wale wale kidato cha sita.
Sekta ya Elimu nchini Tanzania imekuwa ikishuka kila kukicha huku wanafunzi wakizidi kufeli kutokana na mfumo mbovu wa elimu uliowekwa na serikali, Gratian Mukoba ni Rais wa Chama Cha Walimu nchini Tanzania (CWT),akizungumza na Habarimpya.com alisema bajeti ilishapitishwa kwenye bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na fedha zilizotengwa haziwezi kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa sababu mapendekezo ya CWT kama wadau wakubwa wa elimu hayakuingizwa kwenye bajeti hiyo.
Awali Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akizungumza na waandishi wa habari, Dodoma jana alisema kuwa Serikali imetenga kiasi cha Sh18.2 trilioni kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha wa 2013/14. Alisema wameweka vipaumbele kadhaa ambavyo ni nishati vijijini, miundombinu, maji na upatikanaji wa pembejeo za kilimo
No comments:
Post a Comment