WATU wanne wanasemekana kufa kwenye ajali iliyotokea leo majira ya saa
tatu asubuhi eneo la Bwawa la Hatari kijiji cha Dakawa Wilaya ya Mvomero
mkoani Morogoro katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma.
Ajari hiyo iliyohusisha magari matatu ambayo ni lori aina ya Scania,
magari madogo mbili aina ya Prado na Noah, pikipiki ya matairi matatu
'Bajaj' na pikipiki ya matairi mawili aina ya Sanlg.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba watu wanne walikufa papohapo akiwemo dereva wa pikipiki ya matairi mawili.
Mashuhuda walisema chanzo ni dereva wa Noah aliyejaribu kuzipita
pikipiki mbili na lori moja na kwamba Noah hiyo iliyokuwa ikielekea
Dodoma ilipojaribu kuipita Bajaj mbele aliona gari linakuja na kwamba
alifunga breki ghafla na kusababisha dereva wa lori iliyokuwa mbele
yake kuigonga pikipiki (bodaboda) iliyokuwa mbele yake. Hivyo Noah
hiyo ikaikumba Bajaj na kupinduka, ambapo lori nalo lilihama njia na
kwenda porini baada ya kujaribu kukwepa tukio hilo.
Hayo yalisemwa na shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah
Shabani ambaye alikuwa akilima kandokando ya barabara hiyo.
chanzo:.globalpublisher
No comments:
Post a Comment