
Wahu
na Nameless wanategemea kupata mtoto wa piliCouple ya mastaa kutoka
Kenya, Wahu na Nameless inategemea kuungana na couples za mastaa wengine
duniani kama Kim Kardashian na Kanye West, kupokea ujio wa member mpya
katika familia zao kutokana na Wahu kuwa mjamzito wa mtoto wa pili.

Baada
ya kuwepo uvumi kuwa Wahu ni mjauzito wa mtoto wao wa pili, hitmaker
huyo wa ‘Sweet love’ amethibitisha kuwa kweli na anategemea kujifungua
mapema mwezi August mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa facebook Wahu
alimjibu fan mmoja ambaye ni miongoni mwa fans wengi waliokuwa wakitaka
ukweli kuhusu uvumi huo ambao ulithibitishwa kwa jibu lake fupi, “Yes I
am”.
Akiwa
na excitement ya mtoto wa pili Wahu pia anategemea kuachia single mpya
mwishoni mwa wiki hii, wimbo ambao Wahu aliuambia mtandao wa standard
media wa Kenya kuwa itakuwa ni hit song kama ilivyokuwa “Sweet Love” na
“Running Low”.
Mtoto
wa kwanza wa Nameless na Wahu aitwaye Tumiso Nyakwea alizaliwa mwaka
2006 na wimbo wa “Sweet Love” ulikuwa ni dedication kutoka kwa mama
yake, na ni wimbo ambao umemletea matunda ya tuzo kadhaa.

Wanamuziki
na wanandoa hao, walifunga ndoa 2005, ambayo imefanikiwa kutoa majibu
ya mtoto wa kike anayetegemea kupata mdogo wake hivi karibuni.
chanzo bongo61
No comments:
Post a Comment