
BABY MADAHA
Sakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa
kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo
kumfanya awe na haki ya kuhamia.
Akizungumza na mwandishi wetu, juzi jijini Dar es Salaam, Madaha alisema..
pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu pekee ambaye angeweza
kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni tatu) ni Wolper lakini
anamchenga.
“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii mwenzangu alikuwa na
uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini nimemwambia,
ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa. Milioni tatu
ndugu yangu si pesa ndogo.”
KAULI YA WOLPER
Wolper alipotafutwa na kusomewa malalamiko ya Madaha alisema:“Naweza
kusema Madaha hana akili, ni mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara
nyumbani kwangu tungezungumza na baba mwenye nyumba tukajua namna ya
kumsaidia.
“Lakini yeye kabla hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa eti nimemtapeli.
Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment