WAIGIZAJI WA BONGO MOVIE ROSE NDAUKA NA LUCY KOMBA WAMNUNIA MONALISA, KISA JAMAA KUTOKA GHANA.*
MASTAA wa filamu Bongo, Lucy Komba na
Rose Ndauka wanadaiwa kumchunia msanii mwenzao, Yvonne Cheryl ‘Monalisa’
kisa kikitajwa kuwa ni Prodyuza Mghana aitwaye Prince
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba
hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, awali Mona na Prince walikuwa
washikaji na baadaye Mona akamtambulisha Lucy kwa jamaa huyo, hapo ndipo
tatizo lilipoanzia.
“Lucy alipojuana na Prince, akamchukua
Rose kisha wote watatu wakaenda Ghana eti kushuti filamu. Wakiwa huko
sijui walimwaga sumu gani na hapo ndipo uhusiano wa Mona na Prince
ulipoanza kufifia.
“Mona akashangaa ila akapotezea na hata
Lucy na Rose waliporudi hawakuwa wakimchangamkia mwenzao, wakaanza
kumchunia mpaka sasa,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzipata nyeti hizo, mwandishi
wetu alimtafuta Mona ambaye alipopatikana alikiri kuwepo kwa ‘mnuno’
kutoka kwa wasanii wenzake hao, akasema chanzo ni Prince.
“Niliamua kuachana na Prince kwa kuwa
niliona ana tamaa na wasanii na nashangaa Rose na Lucy nao
wanavyonichunia, ingawa kiukweli sikupenda kabisa kuongelea suala hili
kwani sipendi shari,” alisema Mona.
Rose alipoulizwa alikuja juu na kudai hajawahi kuwa na ukaribu na Mona. Lucy hakuweza kupatikana kufungukia madai hayo.
No comments:
Post a Comment