VIGOGO WAWILI WABANWA KUHUSU SUALA LA KUKAMATWA KWA MASOGANGE NA MADAWA YA KULEVYA.
HABARI zilizochimbuliwa kwa undani
zinadai kuwa tayari vigogo wawili waishio nchini wamebanwa na Jeshi la
Polisi Tanzania wakituhumiwa kumtuma Masogange kupeleka madawa ya
kulevya nchini Afrika Kusini.
gnes Gerald 'Masogange' Kwa mujibu wa
habari hizo, vigogo hao (majina tunayo) walidakwa wiki iliyopita kila
mmoja kwa wakati wake na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi
(Central), jijini Dar ambako walihojiwa kwa saa sita.
“Hawa vigogo walikamatwa wiki iliyopita
na kuhojiwa kwa masaa sita, waliachiwa lakini waliambiwa wakihitajika
tena wataitwa,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kikaongeza kuwa, licha ya
kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka, vigogo hao, mmoja alinyang’anywa
‘paspoti’ yake huku mwingine akaunti zake za benki zikifungwa kwa muda
usiojulikana.
Habari zinasema kuwa, kigogo ambaye
akaunti zake zimefungwa amekuwa akihaha kila kukicha kuhakikisha
zinafunguliwa kwa sababu hana njia nyingine ya kuingiza kipato.
Juzi, Ijumaa liliwasiliana na Kamanda wa
Kikosi Maalum cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ili
kujua uhakika wa madai hayo ambapo alisema:
“Sisi (polisi) tumekuwa tukifanya mambo
yetu kwa siri kubwa, si rahisi kusema. Tukisema kunakuwa na ugumu kwa
sababu mnaandika kwenye magazeti, matokeo yake uchunguzi unavurugika.
“Mfano wale wasichana (akina Masogange)
waliokamatwa Afrika Kusini wamekuwa wagumu kuwataja waliowatuma kwa
sababu hao waliowatuma ndiyo wanaowategemea kuwawekea dhamana.”
Agnes Gerald na mwenzake, Melisa Edward
walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Oliver Tambo uliopo Kempton Park nchini humo wakiwa na madawa ya kulevya
aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
No comments:
Post a Comment