Ashanti United Azam FC Coastal Union Habari Kuu JKT Mgambo JKT Oljoro JKTRuvu Kagera Sugar Ligi Kuu Bara Ligi Kuu Tanzania Mbeya City Mtibwa Sugar Prisons R.Shooting Rhino Rangers Simba Sc Tanzania Bara Uhamisho Yanga SC — 07 August 2013
Hatua ya kwanza ya usajili wa wachezaji kwa msimu wa
2013/2014 imefungwa rasmi jana (Agosti 5 mwaka huu) ambapo klabu zote za
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zimewasilisha usajili wa vikosi vyao ndani ya
wakati.
Baadhi ya klabu zimefanya makosa madogo madogo katika usajili
ambapo zimepewa siku ya leo (Agosti 6 mwaka huu) kufanyia marekebisho
kasoro hizo. Hivyo kesho (Agosti 7 mwaka huu) majina ya vikosi vyote
yatabandikwa kwenye mbao za matangazo za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kwa ajili ya kipindi cha pingamizi kitakachomalizika
Agosti 12 mwaka huu.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake
Alex Mgongolwa itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia
uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 14 mwaka huu
ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya
Vodacom msimu huu na wale kutoka nje ya Tanzania. Hivyo, dirisha la
uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya hatua ya pili ya
usajili kumalizika Agosti 29 mwaka huu.
Katika usajili wa wachezaji wapya simba sc na Ashanti united ndizo
timu zilizo tia fora kwa kuwasilisha majina kumi mapya katika vikosi
vyao, huku Azam FC wakiwa wamewasilisha majina matatu toka katika kioksi
chao cha pili (Azam academy)HHII NIDO ORODHA YA WACHEZAJI WAPYA NDANI YA VILABU 14 VINAVYO TARAJI KUANZA MBIO ZA KUSAKA UBINGWA WA TANZANIA BARA 2013/14 AGOSTI 24:
Yanga SC
Hamis Thabit (huru), Deogratius Munishi ‘Dida’ (huru), Hussein Javu
(Mtibwa Sugar), Reliant Lusajo (Machava United, Kilimanjaro), Shaaban
Kondo (huru), Rajabu Zahir (Mtibwa Sugar), Mrisho Ngassa (Azam/Simba).
na Mosses Oloya.
Simba SC
Moses Oloya. Abdulhalim Humoud (huru), Issa Rashid (Mtibwa Sugar)
Ibrahim Hussein (Coastal Union), Adeyoum Saleh (Miembeni,
Zanzibar), Sino Agustino (Prisons Mbeya), Andrew Ntalla (Kagera Sugar),
Joseph Uwino (URA, Uganda), Rahim Juma (huru), Amis Tambwe (Vital’O,
Burundi) na Kaze Gilbert (Vital’O,Burundi).
Azam FC
Hakuna wapya, waliopandishwa toka Azam Academy ni Mudathir Yahya, Aishi Manula na Hamad Juma.
Coastal Union
Juma Nyosso, Haruna Moshi wa Simba na Uhuru Seleiman kutoka Azam,
Kenneth Masumbuko (Polisi, Moro), Crispian Odulla (Bandari, Kenya),
Abdullah Othman (Jamhuri ya Pemba), Marcel Ndaheli na Said Rubawa kutoka
Oljoro JKT ya Arusha.
Mtibwa Sugar
Paul Ngalema, Abdallah Juma kutoka Simba, Said Mohamed aliyetemwa
na Yanga, Salim Mbonde kutoka Oljoro JKT na Ally Shomari aliyekuwa
akikipiga na Polisi Moro iliyoshuka daraja.
Kagera Sugar
Ruvu Shooting
JKT Ruvu
Emmanuel Swita (Toto African), Kalage Gunda (Oljoro JKT) na Salum Machaku (Polisi Moro)
Tanzania Prisons
Wilbert Mweta (Simba)Ibrahim Mamba (Oljoro JKT) na Omega Seme (Yanga, mkopo)
Mbeya City
Paul Nonga (Oljoro JKT), David Abdallah (Prisons Mbeya), Mohamed
Kijuso (huru), Christian Sembuli (Polisi,Dodoma) na John Paul (Polisi,
Moro)
Oljoro JKT
Imemrejesha kundini straika wake Amir Omary aliyetimka mzunguko wa
pili kwa madai ya kutolipwa fedha za usajili wake na kiungo aliyemaliza
mkataba wake na Mtibwa Sugar Babually Seif. Pia, imepandisha vijana 18
kwenye kikosi chake.
Ashanti United
Anthony Matangalu (huru), Issa Kanduru na Salum Malima kutoka
Mgambo JKT, Tumba Sued (huru) Hussein Sued (Ruvu Shooting), Said Maulid
‘SMG’ (huru), Daudi Mwasongwe (Prisons, Mbeya) Raul Magia (Polisi Moro),
Musa Chibwabwa (Villa Squad) na Paulo Maono (Moro United)
Rhino Rangers
Nurdin Bakari na Ladislaus Mbogo kutoka Yanga.
Mgambo JKT
Kocha Mohamed Kampira amesema klabu hiyo haikuwa na fedha za
usajili wachezaji wenye majina makubwa na kuweka nguvu zao kwenye
vijana.
“Tumesajili wachezaji wengi vijana ambao hawana majina katika
soka.Tunataka kutoka nao kutoka huku chini kupanda nao,” alisema Kampira
ambaye amesisitiza kuwa msimu huu watatoa ushindani mkubwa na
wamesajili timu ya kucheza soka la uhakika na kutafuta matokeo si kama
ilivyokuwa misimu iliyopita-kwa hisani ya sportmsuni
No comments:
Post a Comment