Tukio hilo lilitokea Agosti 1, mwaka huu
ambapo mwenye nyumba sambamba na polisi walimkamata Dudu Baya na mkewe
Mariam kwa madai ya kuchoma moto nyumba kwa makusudi na kuwapeleka
katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
“Mkewe alitupia mkaa wa moto katika
sofa, likashika moto kabla majirani hawajanisaidia kuuzima. Baada ya
kuwauliza kulikoni wakanitishia maisha ndipo nikawapeleka polisi na
kupewa RB namba OB/RB/13485/2013 na kuja kumkamata,” alisema Mashaka.
Dudu Baya alipotafutwa na mapaparazi
wetu, alikiri kukamatwa na kuwekwa sero kwa saa sita kabla ya kuwekewa
dhamana na shemeji yake aliyemtaja kwa jina la Vero.
“Vyumba vyake na vyangu haviingiliani
kabisa, tumetenganishwa na ukuta hivyo shutuma zake hazina ukweli dhidi
yetu ila naamini uchunguzi wa polisi ndiyo utatoa majibu,” alisema Dudu
baya
No comments:
Post a Comment