Terethia Fidelis aliyebeba mtoto mgongoni akisindikizwa na umati wa watu
toka ofisi ya mkuu wa mtaa alipokuwa akihijiwa kuhusu tuhuma yake ya
kumpiga, kumpasua kichwani na kumng'ata na meno mgongoni mtoto wake
Magge Fred 8. (PICHA NA JOHN BANDA)
Na John Banda, Dodoma
MTOTO Magge Fred 8 amejuruhiwa kichwani na kung'atwa kwa meno Mgongoni na mabegani na Mama yake mzazi kwa sababu aliiba fedha na kununulia Chips bila ruhusa.
MTOTO Magge Fred 8 amejuruhiwa kichwani na kung'atwa kwa meno Mgongoni na mabegani na Mama yake mzazi kwa sababu aliiba fedha na kununulia Chips bila ruhusa.
Magge
alisema anajisikia maumivu makali kichwani na mgongoni baada ya kupigwa
na mama yake mzazi kutokana na madai ya yeye kutomwambia Dada yake
alipo na chips ambazo mama yake alizikuta chini ya mvungu wa kitanda
tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jumanne hii, inadawa kuwa Theresia Fidelis ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo alimpiga na kumjeruhi mwanae, mwandishi wetu alishuhudia kovu kichwani la kipigo cha kitu kilichomchana na huku mgongoni kukiwa na majeraha kadha ya meno ambavyo vimemsababishia maumivu makali.
Akiongea
mbele ya Mwenyekiti wa mtaa mama wa mtoto huyo alisema aliamua kumpiga
kiasi hicho kutokana na mtoto huyo kumfichia siri Dada yake na pia kuiba
fedha ndani na kununua chipsi pamoja na matumizi mabaya ya anasa.
Theresia
alisema imekuwa ni kawaida kwa mtoto wake huyo Magge Fred 8 kutosema
Dada yake alipo na fedha zinazopotea ndani kutojulikana aliyechukua
badala yake anaona chipsi na vitu vingine vidogo vidogo vya anasa ndiyo
sababu ya kumpiga vibao mpaka kujigonga ukutani na kuchanika kichwani na
kumng'ata kutokana na hasira.
.
.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Karume kata ya Mnadani Matwiga Kyata alisema tukio hilo
lililpofikishwa ofisini kwake aliamua kuchukua hatua za kisheria na
baada ya mahojiano aliamua kuwaita polisi ili sheria ikachukue mkondo
wake zaidi.
Baadhi ya
akina mama waliokuwepo ofisini hapo kushuhudia tukio hilo walisema mtoto
huyo alikimbia toka kwa nyumbani kwao usiku huku akilalama kutaka
kuuawa ndipo waka mpeleka kwa mwenyekiti, pamaja na kulaani kitendo
alichofanya mwanamke mwenzao.
''We
acha hivi unajua uchungu tunaoupata wakati wa kujifungua? kama kweli
aliupata angeweza kufanya hivi mpaka kufikia kumng'ata meno akitaka
kumnyofoa nyama mtoto wake wala haiingii akili labda akapimwe akili la
sivyo achukuliwe hatua kali zinazostahili'', alisema Mwatum Rashid.
Polisi
walithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa
taarifa mapema pindi wanapoona watoto wakifanyiwa vitendo viovu na
wazazi au walezi wao.
No comments:
Post a Comment