Nyota wa Manchester United Wayne Rooney asherehekea baada ya kufunga bao mechi ya awali. Picha/AFP
Na MASHIRIKA
Imepakiwa - Wednesday, July 3
2013 at
07:49
Kwa Mukhtasari
Arsenal
na Chelsea zinatega masikio kwa makini kusikia yanayoendelea kuhusu
straika wa Manchester United, Wayne Rooney baada ya kubainika kuwa
mwanasoka huyo atahama klabu.
LONDON, Uingereza
ARSENAL na
Chelsea zinatega masikio kwa makini kusikia yanayoendelea kuhusu straika
wa ManchesterUnited, Wayne Rooney baada ya kubainika kuwa mwanasoka
huyo atahama klabu Rooney
alitarajiwa kukutana na kocha wake, David Moyes kutatua shida yake ya
kuchoshwa na klabu lakini kulingana na vyombo vya habari nchini
Uingereza, wawili hao walikutana mwezi jana na ilidaiwa kuwa
hawakuafikiana.
Katika
mazungumzo ya wiki hii, Rooney anatarajiwa kufanya uamuzi wake
akisaidiwa na ajenti wake, Paul Stretford na mwenyekiti mpya wa Red
Devils, Ed Woodward.
Moyes
hajakata tamaa kumshawishi Rooney kuipatia Man United nafasi nyingine
lakini kinachosubiriwa sana ni majibu kuhusu ni lini atakapoondoka
mwanasoka huyu, na ni klabu ipi atakayohamia.
Maajenti wake wanatarajiwa kusisitiza kuwa mwanasoka huyo anataka kuhama klabu kufuatia msimu uliopita.
Rooney
alipuuzwa na aliyekuwa kocha, Alex Ferguson kwenye mechi ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid na kushuku ukakamavu wake.
Mwanasoka
huyo pia alichezeshwa katika safu ya kati, kufuatia kuwasili kwa Robin
van Persie ambaye sasa amekuwa chaguo la kwanza la mashambulizi.
United
inajiandaa kwa mechi za kirafiki katika ziara za Mashariki ya Mbali na
Australia juma lijalo na mechi hizi huenda zikawa za mwisho kwa straika
huyo mwenye umri wa miaka 27.
PSG
Rooney
ananyemelewa na mahasimu wa United, Arsenal na Chelsea huku Real Madrid
na Paris Saint-Germain zikiwa macho. Iwapo ataamua kuhama, huenda Moyes
akamwuza kwa klabu nje ya Uingereza, kwani kupeana nyota huyo kwa
Chelsea au Arsenal, itakuwa sawa na kumpa silaha adui.
Kiungo stadi
wa Arsenal, Jack Wilshere ambaye ni Muingereza mwenza wa Rooney amesema
klabu yake itaimarika pakubwa ikifaulu kumnunua.
“Iwapo
itawezekana, basi itakuwa hatua ya kuvutia sana. Rooney ni aina ya
mwanasoka ambaye anaweza kufanya chochote hadi mkashinda taji la Ligi
Kuu. Kumwona katika orodha ya kikosi cha kwanza kunawatia wasiwasi
mahasimu na tunaweza kushinda mataji mengi sana akiwasili,” Wilshere
alisema.
No comments:
Post a Comment