MSANII wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee kivazi chamuumbua katika
tuzo za Tanzania Kilimanjaro Music Awards zilizofanyika mwishoni mwa
wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Msanii huyo alijikuta akishindwa kutembea huku akijiziba mbele kutokana na kigauni alichokuwa amevaa kuwa na mipasuo huku kukiacha sehemu kubwa ya mwili wake. |
Vanessa alionekana kuwa na wasiwasi kila alipopanda jukwaani huku
akiziba mipasuo ya nguo yake ili kuepusha aibu ya kuonyesha mapaja yake
kutokana na mipasuo ya kivazi hicho.
Baadhi ya watazamaji waliofika ukumbini hapo walionekana kushangazwa na kitendo hiko huku wengine wakiohoji kwa nini ameamua kuva hivyo huku akipata wasiwasi wa kuficha sehemu ya mwili wake ili usionekane. "Kwa nini ameamua kuvaa gauni hilo wakati anajua lina mipasuo mirefu ni bora angeacha tu kuliko hivyo anavyopata shida nalo kwa kulishika kuzuia hiyo mipasuo" alisema mdau mmoja aliyehudhuria tuzo hizo |
No comments:
Post a Comment