MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday 19 June 2013

UCHAWI UTATUMALIZA ASEMA CATHY


Mwigizaji wa Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ naye amenyanyua kinywa chake na kuonesha jinsi gani anakerwa na wasanii wanaoshinda kwa waganga ili kutafuta ustaa. Akiongea na mwandishi wetu hivi karibuni, Cathy alisema kuna baadhi ya wasanii (hakuwataja majina) wamekuwa na tabia za kuzunguka kwa waganga wakitafuta kuwa juu katika tasnia ya filamu suala ambalo halipendezi na kuwasihi wawe na hofu ya Mungu. “Vifo vya wasanii vimetokea vingi sana, nilidhani kutokana na vifo hivyo wangepata hofu ya Mungu na kuacha mambo yasiyofaa vikiwemo vitendo vya kishirikina lakini hawakomi, wananikera sana. Ipo siku wataumbuka kwani Mungu siyo binadamu,” alisema Cathy. 
chanzo dorin audax

No comments:

Post a Comment