Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limepata ujumbe kupitia simu
za mkononi ambao umesambazwa kwa wananchi mbalimbali ukisadikishwa kuwa
unatolewa na JWTZ. Ujumbe huo wa simu ya mkononi unasema ‘Habari
zilizotufikia hivi punde. Mtanzania yeyote, kaa makini usiokote kitu
chochote ambacho una shaka nacho, kunabomu zimerushwa toka nchi jirani
Malawi zaidi ya 30 zenye uzito usiopungua tani 100. Hivyo basi uonapo
kitu kipo kama chupa la chai chenye rangi ya fedha. Usiguse’ Piga namba
0756 000042. SMS hii tuma kwa watu uwezavyo. Imetolewa na JWTZ’.
JWTZ linapenda kuwaondoa wananchi hofu kutokana na taarifa hiyo. Kwanza, Ujumbe huo haujatolewa na JWTZ. JWTZ haliwezi likatumia mfumo huo wa SMS kuwapa wananchi wake taarifa za hatari kama hizo. Aidha, JWTZ hutangaza kupitia vyombo rasmi kama vile Magazeti, Radio na Television.
Pili, bomu la tani 100 ni zito mno, halijawahi kutengenezwa duniani. Na kama lipo, haifahamiki bomu hilo litarushwa vipi , kwa kutumia ndege au
Mzinga?. Lakini pia, mzinga wa aina hiyo haupo duniani kote na wala hakuna ndege yenye uwezo huo, hasa kwa bomu lenye umbile dogo kama hilo(Chupa ya Chai).
Tatu, habari hizi hazina ukweli kisayansi wala kiuhalisia au fikra za kawaida. Tunawaomba wananchi wazipuuzie taarifa hizi kwani sio za kweli ni uongo mtupu. JWTZ lipo kwa ajili ya Wanachi hivyo, kwa taarifa hizi za hatari,lazima lingewajulisha wananchi kwa njia zilizoelezwa hapo juu na si kwa simu za mkononi.
Imetolewa na

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment