Jeneza la hayati Mngwear.

Waatanzania wanaoishi Afrika Kusini wakiaga maiti.

Kinje (kati kati) akiwa na watanzania wengine waishio Afrika kusini.

Msanii Bushoke (kushoto) akiwa na mdau aishiye huko Afrika kusini.

Kinje
Ngombale Mwiru akiwa amebeba jeneza pamoja na watanzania wengine huko
Afrika kusini katika juhudi za kusafirisha mwili wa marehemu.
Kamati ya mazishi ya aliyekuwa Msanii wa Bongo Fleva, Albert Mangwea
‘Ngwea’, mpaka jana mchana ilikuwa imekusanya jumla ya Sh milioni 32
kutoka kwa wadau mbalimbali.
Kamati hiyo inahitaji Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia kusafirisha
mwili wa marehemu kutoka Afrika Kusini mpaka Morogoro kwa ajili ya
mazishi. Fedha hizo pia zinahitajika kwa ajili ya kuratibu shughuli
nzima ya mazishi.
Mangwea alifariki dunia Jumanne iliyopita nchini Afrika Kusini akiwa
usingizini kwa madai ya kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya.
Alitarajiwa kuwasili nchini jana lakini kushindwa kutoka kwa ripoti
ya uchunguzi wa madaktari kwa wakati, kumesababisha isijulikane atatua
lini, licha ya kudaiwa kuwa anaweza kutua leo.
Kamati ya Mazishi bado inaendelea na mchakato wa kuratibu shughuli hiyo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi akiwa Mbezi Goig jijini Dar
ambako ndiko kwenye msiba huo, mmoja wa waweka hazina wa kamati hiyo,
Paul Matthysse ‘P-Funk’, alisema mpaka sasa kamati yake imefikisha Sh
32,259,000 ingawa wanatarajia kuendelea kupokea michango mbalimbali
kutoka kwa wadau.
Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa michango yao katika msiba huo ni
P-Funk aliyetoa Sh milioni tano, Clouds Media Group (Sh milioni tano) na
Push Mobile (Sh milioni tano). Kusoma zaidi bofya
Juzi Kampuni ya Global Publishers ilitoa Sh milioni moja.
“Nawasisitiza Watanzania waendelee kutoa michango yao kwa ndugu yao ili kuonyesha umoja tulionao. Fedha zikiwa nyingi tunataka kumfanyia kitu mama yake ili kuendelea kumfariji kwani kipindi hiki ni kigumu kwake,” alisema P-Funk.
“Nawasisitiza Watanzania waendelee kutoa michango yao kwa ndugu yao ili kuonyesha umoja tulionao. Fedha zikiwa nyingi tunataka kumfanyia kitu mama yake ili kuendelea kumfariji kwani kipindi hiki ni kigumu kwake,” alisema P-Funk.
Wakati huohuo jana taarifa zilisema mama mzazi wa Mangwea aishie
Morogoro, Denisia Mangwea, alipandwa na presha baada ya jana kupata
taarifa kuwa mwili wa mwanaye umezuiwa Afrika Kusini kutokana na
uchunguzi wa madawa ya kulevya. Alikimbizwa hospitali na inadaiwa
anaendelea vizuri.
Mangwea aliwahi kutamba na nyimbo kadhaa kali zikiwemo Gheto Langu, She Got a Gwan, Mikasi na Tupo Juu.

No comments:
Post a Comment