MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Saturday 1 June 2013

SAKATA LA KUWANASA WANAOJIUZA LAENDELEA DAR ES SALAAM

 POLISI Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam imeendesha oparesheni maalum ya kuwanasa machangudoa wanaofanya biashara hiyo haramu katika eneo lao na kufanikiwa kuwaweka ‘mtu kati’ makahaba kibao, wakiwemo raia wa Rwanda na Burundi...

Kamatakamata hiyo ilichukua nafasi usiku mnene wa Alhamisi ya Mei 23, mwaka huu kwenye danguro kubwa la makahaba lililopo Kariakoo, jijini Dar ambalo machangu hao hutegea mingo zao kwa ajili ya kuwanasa wateja.

Katika hali iliyowashangaza polisi, midume iliyokutwa na makahaba hao ilitimua mbio ili kujiokoa na mtego huo wa polisi uliodhamiria kusafisha eneo la Kariakoo kwa ukahaba uliopitiliza.


Baadhi ya wanaume wakati wakitimua mbio walisikika wakisema kuwa wakukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola ni wanawake hao kwa vile wanavaa kimitego huku wakijua binadamu anapitiwa na shetani wakati wowote.

“Sisi kosa letu nini? Wakamateni haohao machangudoa, watavaaje kimitego mbele yetu sisi wanaume? Shetani naye atakuwa wapi wakati huo?” alisikika akisema mmoja wa wanaume hao huku akichanganya miguu kupita kawaida.
 
Awali kabla ya zoezi la kuwanasa makahaba hao halijaanza, afande mmoja alipowauliza wanachofanya hapo, kahaba mmoja aliuliza: Una maswali mengi kwani we ni polisi?

Mei 24, mwaka huu, makahaba hao walipandishwa kwenye Mahakama ya Jiji na kusomewa mashitaka yao na mwendesha mashitaka, John Kijumbe mbele ya Hakimu Timoth Lyoni.

Waliosomewa mashitaka ni Natasha Bahati, 30 (Mrundi), Asma Athuman, 23 (Mrundi), Niyonkuru  Evelinde, 29 (Mnyarwanda), Zaimana Hawa, 20 (Mrundi) na Wabongo 35.
 
Wote walikana mashitaka lakini walipelekwa Gereza la Segerea, jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

No comments:

Post a Comment