MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Saturday 1 June 2013

HII NI SIRI KUBWA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA KIFO CHA ALBERT MANGWEA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjmk_nDUsMlVTumIt6aNatupM6O9lCmsFyjD8c_d2Jf4ULSZpSnzdKj5Kxsg-0hv8o8zGxMu7n09OxodcDMY4f3QN6-D1ewkvYJNni3dHlsoGRKA7z7Oke1tfUxDDFhWzGKTGwfXec07e4e/s1600/14.JPG 
Pretoria,Afrika Kusini
WATANZANIA wanaoishi nchini Afrika Kusini na nchi jirani ya Botswana leo wamejitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea,kesho mwili wa marehemu unatarajia kuwasili nchini Tanzania na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa, kabla ya shuguli za kuuaga tena kufanyika katika Viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Mangwea aliagwa na umati wa watu mbalimbali wakiwemo Watanzania na watu wa mataifa mbalimbali wanaoishi nchini Afrika Kusini, jijini Dar es Salaam pia kutakuwa na zoezi kama hilo siku ya Jumatatu kabla ya kusafirishwa hadi mjini Morogoro kwa mazishi siku ya Jumanne.

Pamoja na kwamba Mangwea anatarajia kuzikwa mjini Morogoro, utata juu ya ripoti ya uchunguzi wa kifo chake imeanza kutawala, baada ya kuwepo kwa mvutano wa kuifanya ripoti hiyo kuwa siri, huku baadhi ya watu wakitaka ripoti itangazwe kama ilivyoandikwa na jopo la Madaktari wa Hospitali ya  St Hellena Joseph.

Inaelezwa kwamba familia ya msanii huyo imekataa kuweka wazi sababu za kifo cha mtoto wao, "Ripoti ya Uchunguzi wa Madaktari imetoka lakini haturuhusiwi kuitoa kwa sababu ndugu zake wamekataa, ila kuiona nimeiona na siwezi kukwambia kwamba inasemaje"alisema mmoja wa watu wa karibu wanaoshugulikia taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuja nchini Tanzania katika mahojiano maalumu na Habarimpya.com.

Habarimpya.com pia ilijaribu kuwasiliana na ndugu na jamaa wa Ngwea nchini Tanzania na kudai kwamba, ni kweli ripoti ya uchunguzo wa Madaktai umetoka lakini wao kama familia hawajaiona.  

"Nikweli tumesikia hivyo, lakini hatujui chochote kilichoandikwa na Madaktari, hivyo hatuwezi kuizungumzia, ingawa mimi pia siyo msemaji wa familia, lakini hata ukiwaona wahusika bado hawatakuwa na majibu yoyote kwa sababu wao wako Tanzania na ripoti bado iko Afrika Kusini"alisema mmoja wa wanafamilia wa marehemu ambaye hakutaja jina lake liandikwe ndani ya mtandao wa Habarimpya.com.

No comments:

Post a Comment