
MWIGIZAJI
Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper ‘Wolper
Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni
waume za watu, kwa hiyo kwa kuwa nao si rahisi kuonyesha mapenzi yao ya
dhati kwake kwani mapenzi yao ni chumbani tu, lakini hawezi kutembea
nao hadharani kwa kuhofia ndoa zao.


“Wengi watu wenye pesa zao kuna wakati wananiona nina dharau lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke ya mtu anayenijali na kuwa karibu na mimi sasa kuna watu wanaamini pesa zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau”,anasema Wolper Gambe.
Aidha kuna watu ambao uwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na wanaroho kama wanadamu wengine wao si malaika wanapenda na kupendwa, kwa hiyo ukimuona ana kijana Serengetiboy ujue ni kwa ajili ya kupata penzi nzito na kusikilizwa haja zake.
No comments:
Post a Comment