MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday 26 June 2013

AFARIKI DUNIA SIKU CHACHE BAADA YA KUBAKWA NA WAVULANA WANNE...NI BINTI WA MIAKA 10

Wanawake wakiandamana mitaani kulaani vikali vitendo vya ubakaji nchini humo.
Binti mmoja mwenye umri wa miaka 10 amefariki dunia siku chache baada ya kubakwa na kundi la wavulana wanne mjini Mumbai, polisi walisema jana.

Msichana huyo alisemekana kuwa alipelekwa kwenye eneo lisilojulikana huko Hanuman Nagar baada ya watuhumiwa waliomshambulia - ambao wanasadikika kuwa na umri wa kati ya miaka 13 na 16 na wawili kati yao wakiwa ndugu - walimuahidi kumpatia Rupia 10 kama angewafanyia kazi ndogo.
Maofisa mjini Turbhe walisema msichana huyo mdogo aliwafahamu wavulana hao wote wanne waliomshambulia, na kwamba mmoja alimbaka katika tukio jingine siku zilizopita.
Muathirika huyo anaaminika kuwa alikimbizwa hospitali moja mjini Vashi baada ya kupatwa na homa kali siku nne baada ya shambulio lake Juni 16 huko Hanuman Nagar.
Hali yake ilipozidi kuwa mbaya alihamishiwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi cha Hospitali ya DY Patil mjini Nerul, ambako alifariki dunia juzi, imeripotiwa.
Kwa mujibu wa ripoti polisi wa eneo hilo alisema msichana huyo alielezea mateso yake kwa mmoja wa marafiki zake, ambaye naye akawaeleza wazazi wake Jumatatu.
Ofisa mmoja anayefanyia kituo cha polisi cha Turbhe alieleza: "Watuhumiwa wote wanafahamiana pia wanamfahamu binti huyo. Walimbaka kwa kurudia-rudia.
Alipelekwa hospitalini baada ya wazazi wake kugundua kuhusu mkasa wake lakini akapoteza maisha yake Jumanne," alisema.
Watuhumiwa wote wanne wamekamatwa, imesema ripoti hiyo.
Mfululizo wa matukio ya kutisha ya ubakaji nchini India yametawala vichwa vya habari katika miezi ya hivi karibuni, likiwamo lile shambulio baya zaidi dhidi ya mwanafunzi mwenye miaka 23 ndani ya basi Desemba mwaka jana.
Msichana huyo alifariki kwenye hospitali moja nchini Singapore kutokana na majeraha yake wiki mbili baada ya shambulio hilo, ambalo liliwakera sehemu kubwa ya jamii ya Wahindi.
Maelfu ya waandamanaji walivamia mitaa siku kadhaa baada ya shambulio hilo kuonesha hasira yao juu ya uhalifu dhidi ya wanawake nchini India.
Mapema mwezi huu mtalii kutoak Ireland mwenye umri wa miaka 21 alidaiwa kukokotwa na kubakwa wakati akiwa katika kazi za kujitolea mjini Kolkata na taasisi yake ya misaada.
Siku moja tu baadaye, polisi walisema mwanamke mmoja wa Marekani mwenye miaka 30 alibakwa na wanaume watatu wakati akitembea kuelekea nyumba moja ya wageni kaskazini mwa hoteli ya India ya Manali.
Pia mwezi huu wanawake na wanafunzi walivamia mitaa mjini Barasat kupinga kubakwa na kuuawa kwa mwanafunzi mmoja wa chuo mwenye miaka 20.
Mwezi Machi wanaume sita walifikishwa mahakamani nchini India wakidaiwa kumbaka mtalii wa Uswisi na kumpiga mumewe kwa fimbo wakati wanandoa hao waliokuwa mapumzikoni wakiendesha baiskeli huko Madhya Pradesh.

No comments:

Post a Comment