Jeshi
la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na
maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu
kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea
kwenye viwanja hivyo .
Akizungumza
ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema
kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo
imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu
upelelezi.
Kamanda Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.
Hali
kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi
wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya
kuomboleza ..
Hata
hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo
hilo na kuanza kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA ,
hali iliyoleta mvutano kati ya
viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao.
No comments:
Post a Comment