JESHI la Polisi Mkoani Mbeya
linamshikilia Mwalimu wa Masomo ya Ziada akituhumiwa kumbaka Mwanafunzi
wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 10.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
lilitokea Hivi karibunikatika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa
Mbeya.
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa
ni Ipyana Gidion(30),kyusa,mkulima mwalimu wa masomo ya ziada (tuition)
katika kituo cha Itunge Moravian mtaa wa Mbugani Wilayani Kyela Mkoani hapa.
Alisema Mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka 10, kyusa,mwanafunzi darasa la nne katika Shule ya msingi Mbugani mkazi wa Itunge “a” na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Kamanda Diwani alisema mbinu iliyotumika ni kuwaruhusu wanafunzi aliokuwa akiwafundisha kuondoka na kubaki na mhanga kisha kumbaka katika chumba anachotumia kufundishia (darasani).
Aliongeza kuwa mtuhumiwa aliwahi
kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kutoka
kwa rufaa na kwamba mhanga amepatiwa matibabu na kuruhusiwa ambapo
taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.
No comments:
Post a Comment