KATIKA
hali ya kusikitisha jamaa mmoja mkazi wa majengo mjini Moshi
anayefahamika kwa jina la Frank Ngowi amegongwa na Hiace (daladala)
yenye nambari za usajili T352 AFM inayofanya safari zake za
kutoka Kiboriloni mpaka mjini Moshi. Ajali hiyo iliyotokea maeneo ya
majengo polisi karibu na Kishamba Dispensary imesababishwa na dereva
aliyekua akiendesha daladala hiyo kulewa kupita kiasi. Dereva huyo wa
daladala ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa haraka alipogundua
amesha sababisha ajali alikimbia na kuelekea maeneo ya majengo secondary
ambapo waendesha bodaboda walimkimbiza na kufanikiwa kumkamata na
kumrudisha mpaka kwenye eneo la ajali.
Huyu ndiye Frank Ngowi muendesha baiskeli aliyegongwa na daladala, akionyesha jinsi alivyoumia baada ya kugongwa na daladala.
Hii ndio daladala iliyosababisha ajali na kukimbia lakini ilikamatwa na kurudishwa mpaka katika eneo la ajali..
Mashuhuda wa ajali hiyo wakiwa katika eneo la ajali.
Hawa ndio vijana waliomkimbiza dereva wa daladala hadi kumkamata na hapo ndio wapo kwenye harakati za kumrudisha kwenye eneo la ajali.
Gari ya polisi ikiwa imesha wasili katika eneo la ajali, likiwa na askari wa usalama barabarani tayari kupima ajali.
No comments:
Post a Comment