MAHAKAMA ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida umemhukumu mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Kisana wilayani humo, Sayuni Ramadhani (42) kwenda jela miaka mitatu baada ya kukiri kosa la kumng’ata mumewe sehemu zake za siri.
Mwendesha
mashitaka mkaguzi wa polisi, Vincent Ndasa alidai mbele ya hakimu
mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Iramba, Kariho Mrisho kuwa Juni 4
mwaka huu saa 12.00 jioni katika kijiji cha Kisana, mshitakiwa kwa makusudi alizing’ata kwa meno sehemu za siri za mume wake, Onesmo Nathania (42) na kumsababishia maumivu.
Ndasa alidai kuwa siku ya tukio, wanandoa
hao waliporejea nyumbani kutoka kwenye klabu cha pombe ya kienyeji
kijijini hao, kulitokea kutokuelewana na hivyo kuanza kugombana.
Alidai wakati wanaendelea kupigana, Onesmo alizidiwa nguvu na kuangushwa chini na mkewe ambaye alifungua zipu ya suruali na kufanikiwa kuzitoa sehemu za siri za mumewe na kuzing'ata nusura azitenganishe.

mashitaka aliendelea kudai kuwa mlalamikaji Onesmo alipiga yowe na
majirani walifika mara moja na kumkimbiza katika zahanati ya kijiji kwa
ajili ya matibabu.
Mshitakiwa
alipoulizwa iwapo ni kweli alikiri kosa na akaiomba mahakama imwonee
huruma kwa kumpa adhabu ndogo kwa kuwa hilo lilikuwa ni kosa lake la
kwanza na kwamba anahitaji kuwa na mumewe ili waendelee kulea idadi
kubwa ya watoto wao kwa pamoja.
Naye mwendesha mashitaka, Ndasa aliiomba mahakama kumpa adhabu kali mshitakiwa ili kuwa fundisho kwake na pia kuogopa wanawake wanaotarajia kuwafanyia unyama wa aina hii wa kung’ata sehemu nyeti za waume zao.

Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Mrisho, alisema mahakama yake imezingatia
kwa makini maombolezo ya mshitakiwa na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya
kutumikia jela miaka mitatu.
Source:habari le
Source:habari le
No comments:
Post a Comment