MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday, 17 April 2013

Mgambo yatia Nuksi Ubingwa


Ligi kuu Tanzania bara iliendelea leo, huku vita kubwa ikiwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jijjini Tanga ilipoikutanisha Yanga na Mgambo Fc.
Wakicheza kwa presha kubwa kuhitaji pointi muhimu sana ili kukalibia kutangaza Ubingwa mapema,Yanga walijikuta wakipata sare ya goli moja kwa moja.
Mgambo ndio walikua wa kwanza kupata bao kabla ya Msuva kusawazisha dakika ya 87 na kuisaidia timu yake kuepuka kipigo kabisa, kwa matokeo hayo sasa Yanga wanahitaji pointi nne tu ili kutangaza ubingwa kwani watafikia pointi 57 ambazo wapinzani wao wakubwa msimu huu Azam Fc hawawezi kizifikia.
Matokeo ya mechi nyingine Mtibwa waliifunga JKT Oljoro goli moja bila majibu pia Kagera Sugar ilikua ikiongoza goli moja bila majibu dhidi ya Toto Afrika inayopigana kutoshuka daraja.
Sasa ligi ipo ukingoni zikiwa zimebaki mechi chache kwa kila timu.
Msimamo wa ligi Kuu.

#   Team MP W D L GoalsGD Pts
1 Yanga SC 23 16 5 2 4027 53
2 Azam FC 23 14 5 4 4122 47
3 Kagera S 23 11 7 5 258 40
4 Simba SC 22 9 9 4 3211 36
5 Mtibwa S 24 9 9 6 263 36
6 Coastal U 22 8 8 6 233 32
7 JKT Oljoro 24 8 7 9 23-4 31
8 R.Shooting 21 8 4 9 21-1 28
9 Prisons 23 6 8 9 14-7 26
10 Mgambo 23 7 4 12 16-6 25
11 Toto 24 4 10 10 21-11 22
12 JKTRuvu 21 5 5 11 18-15 20
13 Polisi M 22 3 9 10 12-10 18
14 A.Lyon 23 4 4 15 16-20 16

No comments:

Post a Comment