Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo tarehe 17
April, 2013 imekutana na ujumbe wa FIFA ulioongozwa na Bw. Primo Corvaro ambao
umekuja Wizarani kwa ajili ya kujitaMbulisha. Ujumbe huo umekutana na Katibu
Mkuu, Bw. sethi Kamuhanda kwa niaba ya Waziri Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
ambaye yuko safarini.
Katika utambulisho huo, ujumbe wa FIFA umemweleza Katibu Mkuu
kwamba wamekuja kufanya tathmini ya matukio yaliyojitokeza wakati mchakato wa
uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).
Wameeleza kwamba tathmini yao itajikita katika Kukusanya
taarifa mbambali kutoka kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya wagombea
walioenguliwa na kisha kuwasilisha maoni na uchambuzi wao Makao Makuu ya FIFA
mjini Zurich, Uswisi kwa majadiliano zaidi na baadaye kutoa ushauri wa
namna ya kumaliza changamoto iliyopo.
Aidha, ujumbe huo umeeleza kwamba walilazimika kuja nchini
Tanzania baada ya ya kupata malalamiko kutoka kwa wagombea walioenguliwa katika
kinyang'anyiro cha uongozi na baadaye kuombwa na TFF kuja kuwasikiliza
walalamikaji.
Akipokea salaam zao, Katibu Mkuu kwa niaba ya Waziri
aliushukuru ujumbe huo kwa ujio wao ambao alsema anaamini utaweka mazingira
rafiki ili uchaguzi ufanyike bila malalako tena. Aidha ailishukuru FIFA kwa
mchango mkubwa inaotoa kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Aliwahakikishia wajumbe hao kwamba serikali yetu itaendelea
kushirikian na FIFA kwa ari na mali ili kuhakikisha mpira unasonga mbele kwa
amani na utulivu.
No comments:
Post a Comment