MATANGAZO
Sunday, 7 April 2013
HUU NI UJIO MPYA WA MSANII ZAX B KUTOKA MBEYA NYIMBO MAMA NISAFIRISHE
Msanii Zax B anayefanya vizuri sana pande za nyanda za juu kusini katika
anga ya muziki wa bongo flava maskani yake yakiwa jijini Mbeya
akiwakilisha kundi la Homestigers ambao wanafanya vizuri mbeya anawaomba
mashabiki wake wampokee vizuri kwa ujio mpya wa ngoma yake kali
inayoitwa Mama nisafirishe baada ya kimya cha muda mrefu.Baada ya
kuhojiana naye pande za Mbeya mjini na hicho ndicho alichosema."yap
mziki nimeanza zamani lakini ndo hivyo kama unavyoisikia nyimbo hii
kiukweli iko vizuli na hii ni baada ya ile nyimbo yangu ya mwisho
iliyofanya vizuri pia iliotambulika kwa jina la napenda muziki, na
kikubwa ni support kutoka kwa mashabiki ambao wanafeel mziki wangu na
naamini mambo yatakuwa vizuri tuu kwani nakalibia kumaliza video ya
nyimbo hii ili kukamilisha album yangu itayofahamika kwa jina la mama
nisafilishe".Alisema Zax B
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment