Kwa mara nyingine club ya fc barcelona imefanikiwa kuingioa nusu fainal ya michuano ya club bingwa barani ulaya kwa faida ya goli la ugenini baada ya kulazimishwa sare ya goli moja kwa moja na psg ya nchini ufaransa.
katika uchezo wa jana uliopigwa kwenye dimba la nou camp ncchi uhispania psg ndio walikua wa kwanza kujipatia bao kupitia kwa winga wake wa kushoto javier pastore dakika ya 49 kabla ya pedro kuzima ndoto ya wafaransa hao katika dakika ya 71 baada ya kuisawazishia timu yake goli.
kwa matokeo hayo barcelona imefanikiwa kusonga mbele kwa faida ya goli la ugenini kutokana na matokeo ya mchezo wa awali ambapo timu hizo zilifungana kwa mabao 2 kwa 2.
MATUKIO KATIKA PICHA
Barcelona wakishangilia kuingia nusu fainali
pedro akifunga bao la kusawazisha dk ya 71 lililoiwezesha barca kusonga mbele
gerald pique akishangilia na wachezaji wenzake
ibrahimovic akiwa na wenzake wakitafakari namna walivyotolewa
TIMU ZILIZOFANIKIWA KUINGIA NUSU FAINALI
Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, Borussia Dortmund
ni timu zinazowakilisha nchi mbili za ujerumani na spain, ambapo zinasubiri droo itakayochezeshwa siku ya kesho ijumaa kufahamu nani atapambana na nani.
ni timu zinazowakilisha nchi mbili za ujerumani na spain, ambapo zinasubiri droo itakayochezeshwa siku ya kesho ijumaa kufahamu nani atapambana na nani.
Super sub: lionel messi akiingia kuchukua nafasi ya ces fabrigas dk ya 62 na kwenda kubadili matokeo ya mchezo
javier pastore akiifungia psg goli mbele ya dan alves

No comments:
Post a Comment