MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Saturday 22 July 2017

AJALI MBAYA YA DALADALA NA TRENI YATOKEA TENA DAR

Wawili Wafariki kwa Ajali ya Daladala Kugonga Treni, Dar


Ajali ya treni.

Watu wawili wamekufa na wengine 36 kujeruhiwa katika  ajali iliyotokea leo asubuhi ikihusisha gari ya abiria aina ya coaster kukigonga kichwa cha treni maeneo ya Yombo Devis Kona, Temeke jijini Dar.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto amesema  watu wawili wamefariki dunia akiwamo mwanamke mmoja na mwanaume mmoja ambaye ni kondakta wa daladala hiyo.
Muroto amesema mbali na watu wawili kufariki pia kuna majeruhi 36 wanne kati yao wakiwa mahututi.
Amesema majeruhi mahututi ni wanawake watatu na mwanaume mmoja.
“Majeruhi wite wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke na miongoni mwa majeruhi hao wanne wapo katika hali mbaya”amesema Kamanda Muroto.

source global publishers

No comments:

Post a Comment