MBEYA: WAKAZI wa eneo la Isanga katika Jiji la Mbeya
wameendelea kushuhudia visa, mikasa na matukio ya vioja, baada ya mtoto
HARUN JAILO KYANDO mwenye umri wa miaka 9 aliyedaiwa kufariki na mwili
wake kuzikwa jana kwenye makaburi ya Isanga jijini humo ambapo baadaye
alikutwa akiwa kitandani kwake amelala usingizi mara baada ya wazazi na
ndugu kurejea kutoka makaburini.
Wananchi wakiwa wamejaa makaburini kushuhudia tukio la kufukua jeneza hilo.
Mara baada ya kufika nyumbani familia
ikiwa inaingia ndani mwao, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao
akiwa amelala fofofo kitandani kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha
mtoto huyo aliamka na kuonekana akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.
Jeneza mara baada ya kufukuliwa.
Kwa pamoja wananchi na wanafamilia
walikubaliana asubuhiya leo kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini
kilichozikwa, na hivi dakika hizi zoezi hilo linaendelea na picha za
makaburini hapo.
Jeneza hilo likibebwa na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
limesimamia zoezi zima la kufukua jeneza hilo na baada ya kumalizika
kwa shughuli hiyo, kilichokutwa ni jeneza tupu likiwa halina kitu
chochote.
Source:global publishers
No comments:
Post a Comment