Stori: Hamida Hassan
WAKATI
dunia ikiingia Mwaka Mpya wa 2015, taarifa ikufikie kwamba kigogo mmoja
ambaye ni mfanyabiashara maarufu jijini Dar amewaangushia wanaye,
Hassan na Khadija Dilunga sherehe ya kuzaliwa ambayo imepachikwa jina la
‘Escrow’ kufuatia kufuru ya fedha iliyooneshwa na wahusika hivyo kuwa
ndiyo gumzo la mjini kwa wikiendi iliyopita.
Bethidei ya Hassan na Khadija Dilunga wakiwa na makapu ya fedha.
MSHANGAO!
Sherehe hiyo ilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Msasani Tower jijini Dar
juzi ambapo waalikwa wengi walijikuta wakibaki midomo wazi kwa vile
wakati wanafika nje walijua ni harusi ya mtoto wa mtu mzito serikalini
lakini walipozama ndani walipigwa butwaa kukuta ni ‘bethidei’.
“Du!
Ni sherehe ya aina yake, watoto wameingia kama maharusi kwa kumwagiwa
maua tena wana ‘meidsi’ na upambaji wa ukumbi unatisha, naona
umesheheni mapambo ya gharama kubwa,” alisikika akisema mwalikwa mmoja
huku akiendelea kushangaa maandalizi hayo ya kukata na mundu kama si
shoka!
KULA, KUNYWA ZAIDI YA HARUSINI
Taarifa zaidi zinasema kuwa, waalikwa walikula vyakula vya kila aina
tena vya gharama. Walikunywa mvinyo wa bei mbaya na vitu vilikuwa vya
kumwaga kuliko hata inavyokuwa harusini.”
Keki za kifahari na shampeni kibao.
WABADILI NGUO UKUMBINI
Kama vile haitoshi, watoto hao wakiwa ukumbini hapo huku wakikata keki
kubwa na kulisha wazazi na wageni waalikwa, kuna wakati walikwenda
kubadilisha nguo ambapo kama mwalikwa aliwaona wakati wanaingia, ilikuwa
tofauti na wakati wa kutoka. Hassan kwa juu alivaa T-shirt iliyoandikwa
Air Jordan ambapo ilikuwa sare na ya baba yake aliyevaa naye Air
Jordan.
JEURI YA FEDHA
Lilipowadia suala la kutuza sasa, watoto hao walimwagiwa mifedha hasa
noti nyekundu (msimbazi) na madolari (dola) hadi wakajaza vikapu viwili
walivyovishika mapajani. Hata hivyo, haikujulikana kiasi cha pesa
kilichopatikana!
ZAMU YA MAMA WATOTO SASA
Mama huyo wa watoto hao (Tunt) naye ilipofika zamu yake ya kutoa
zawadi, aliwapa simu aina ya Sumsung Galax note 3 na mikufu ya dhahabu
ambayo kwa mwonekano ni kuanzia gramu tano na kuendelea.
Waalikwa wakifungasha fedha ukumbini.
FUKO LA FEDHA
Katika hali ya kushangaza, mama huyo alijaza fedha kwenye FUKO LA RAMBO
na kuondoka nalo, utadhani ilivyokuwa kwa waliochota fedha kwenye
Akaunti ya Tegeta Escrow ambayo kwa sasa ni gumzo nchini kote.
“Jamani
naona leo hapa ni kama Escrow kwa kwenda mbele. Hebu angalia ule mfuko
ya rambo, umejaa fedha. Sijui ndiyo mifuko aina ya sandalusi aliyoisema
Zitto Kabwe? (mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali).
Mmoja wa waalikwa akiwa na rambo la fedha.
RASHIDA WANJARA NDANI
Katika sherehe hiyo iliyokuwa na watoto wengi wa mjini, staa pekee
aliyeshaini ni aliyekuwa Miss Mara 2000/01, Rashida Wanjara ambaye
alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
HAIJAWAHI KUTOKEA
Akizungumzia shughuli hiyo, Wanjara alisema kwamba haijawahi kutokea
sherehe ya kuzaliwa kuwa vile na kutikisa jijini Dar kwani watu walikula
na kujiachia na kilichotikisa zaidi ni fedha zilizomwagwa ukumbini
hapo.
“Kiukweli mihela
ilinifanya nishangae kwani mama shughuli aliondoka na mfuko wa rambo wa
fedha ambao uliwashangaza watu wengi ni kwa jinsi alivyotunzwa, lakini
pia kuna marafiki wa mama shughuli nao niliwaona wakibeba fuko la fedha
kichwani,” alisema Rashida.
Waalikwa wakigonga chiazi.
MASWALI YA WAALIKWA
Baadhi ya waalikwa wa shughuli hiyo walikuwa wakiulizana kuwa, kama
sherehe ya kuzaliwa kwa watoto ‘kufuru’ inakuwa vile, je kwenye harusi
itakuwa vipi?!“Sasa jamani, hii bethidei ndiyo makamuzi yote haya,
msosi, vinywaji, mafwedha. Je, siku ya harusi ya mtoto mmoja kati yao
itakuwaje?” alihoji mwalikwa mmoja bila kujua paparazi alikuwa jirani
yake.
BENDI YA TAARABU YAHUSIKA
Kwa upande wa burudani, Bendi ya Taarab ya Ustadhi ilihusika ambapo
ilitumbuiza na kukonga vilivyo nyoyo za wageni waalikwa ambao waliondoka
ukumbini hapo wakiwa vizuri. Picha ni kwa msaada wa Mashughuli Blog.
No comments:
Post a Comment