Kijana mmoja
anayeaminika kuwa shabiki wa Manchester United Football Club amejiua
jana usiku jijini Nairobi baada ya timu yake kufungwa 1-0 to Newcastle.
Polisi
imesema kwamba John Jimmy Macharia, 23, alijirusha kutoka ghorofa ya 7
baada ya kujua timu yake imepoteza mchezo wa jana jioni. Kwa mujibu wa
mkuu wa polisi jiji la Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia rafiki
zake hawezi kuendelea kuangalia timu yake ikifungwa kila siku kabla ya
kuruka ghorofani. “Mashahidi
wote waliokuwepo wakati wa tukio bado wapo mikononi mwa polisi
wanahojiwa,” alisema. Kibue aliwashauri vijana wa jiji la Nairobi
kufahamu English Premier League ni mchezo tu kama ilivyo michezo mingine
na hivyo waache kuchukua hatua za namna hii kisa michezo. Hii si mara
ya kwanza kwa kwa kijana kupoteza maisha kwa ajili ya michezo
inayochezwa England,” alisema Kibue.
No comments:
Post a Comment