ZIJUE SABABU ZINAZO WAFANYA DADA ZETU KUVAA NGUO FUPI, BASI SOMA HAPA
Wakati mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake
wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa
wanaume. Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini
wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba
wanamapungufu kwa mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri
inabidi kuziba pengo au udhaifu huo. Wakati mwingine hata wanawake
wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi
zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro
fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au
inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na
kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri. Udhaifu
wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma
ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale
maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. Kuyatangaza huko
humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa
sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa. Hebu angalia wanawake
ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara
nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya. Huvaa
nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni
wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata
wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo. Wengi hawavai tu nguo
hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio
la udhaifu wao
No comments:
Post a Comment