Saynag katika pozi.
Hitmaker wa Inatosha, Nafsi inauma
SAYNAG ABRIHHAN a.k.a SAYNAG amesema sababu za ukimya wake katika gemu
umetokana na matatizo ya kifamilia baada ya kufiwa na Mama yake mzazi.
Akipiga stori na Chumba Cha Sindano
kupitia Kipindi cha Kali za Bomba cha Kituo cha redio Bomba FM Mbeya, SAYNAG ameeleza
kuwa “kuna watu wanajua mimi nilifikwa na matatizo na msiba, kuna wengine
hawajui hilo suala yaani yote hayo ni kutokana na matatizo ambayo marehemu mama
yangu alikuwa nayo. Kwanza alikuwa anaumwa sana kwa hiyo nilikuwa sina muda wa
kuingia studio kurekodi, kichwa change chote kilikuwa kina muwaza kwanza mama
yangu, nilikuwa nataka apate afueni kwanza halafu niendelee na kazi zangu
lakini haikuwa riziki kwa hiyo pia nikazindi kuchanganyikiwa kwamba nimemkosa
pamoja na jitihada zangu, sikuwa na muda wa kufikiria kutoa nyimbo kwa wakate
ule, sikuwa na muda wa kufikiria show, siku na muda wa kufikiria chochote zaidi
ya kile kitu ambacho kilichokuwa kinaniumiza,
lakini hayazoeleki ila kutokana na hali halisi inabidi nikubaliane na
hali halisi ilivyo kwa sasa inabidi niendelee tu na kazi zangu, lakini ni mtu
aliyekuwa ananipa sapoti kubwa katika kazi zangu”.
Aidha SAYNAG amesema kuna changamoto
nyingi ambapo kwa baadhi ya wasanii wenzake wenye menejimenti za uhakika wapo
radhi wamzipe mtu Fulani atoke mtu Fulani kwa ushwawishi wa nyimbo kutopata
airtime katika vituo vya redio na Tv kwa wasanii wengine wasio na menejimenti.
“Lakini naamini kama wewe msanii unajua nini unachokifanya
unaendelea tu kufanya kama mimi au watu wengine ambao hawasimamiwi au
wanajisimamia mwenyewe, Kipaji mimi kama nakipaji changu najiamini sehemu wowote hata kama mtu
ataamua anizibe mimi lakini still wapo wanaokubali na wanataka uwepo kila siku
siangalii nani yupo chini nani yupo juu mimi naangalia kazi yangu na mashabiki
wanahitaji kitu gani, mara nyingi nilikuwa nasikia sana mashabiki wanalalamika
kwenye mainternet kwamba sijatoa nyimbo mbona niko kimya, wanaona kama nimeacha
gemu ni kipaji ambacho ninacho mwenyewe yaani, sifosiwi namaanisha sitafuti mtu
anitungie, kwa maana kwamba amesusa kunitungia sasa hivi wimbo, kwa hiyo nimeamua kunyamazwa kwa
sababu sinanyimbo ya kutoa hapana, natunga mwenyewe natafuta melody mwenyewe,
kwa hiyo ni kitu ambacho ninacho milele siwezi kukiacha kwa hiyo wao wasubirie
tu sasa hivi nipo vizuri nitaachia track niliyomshirikisha BEKA sambamba na
video niliyofanya na BLUE.
No comments:
Post a Comment