Wapiganaji wa Kiislamu wa Al
Shabaab nchini Somali wamesema wao ndio waliotekeleza shambulizi la bomu
la kujitoa muhanga nje ya hoteli katika mji mkuu wa Mogadishu nchini
Somalia ambapo watu sita waliuawa wakiwemo maafisa wa polisi.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amelaani
shambulio hilo lilitokea nje ya Hotel ya Maka al Mukurama huku
akisisitiza kuwa shambulio halitarudisha nyuma jihada kubwa
zinazoendelea za kuleta amani na usalama nchini humo.
Kundi hilo la Al Shabaab ambalo lilifurushwa na majeshi ya Somalia yakishirikiana na yale ya Umoja wa Mataifa AMISOM miaka miwili iliyopita wameapa kuendeleza harakati zao za kufanya mashambulizi.
Hapo awali Waziri wa Mambo ya ndani wa Somalia Abdikarim Hussein Guled aliiambia BBC kuwa watu sita waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga.
Mwandishi wa BBC Ibrahim Mohamed Adan ambaye yupo Mogadishu amesema sauti ya mlipuko ulisikika katikati ya mji huo wa Mogadishu.
-BBC

No comments:
Post a Comment