SHULE ya Sekondari Nguvumali wilayani Tanga, inadaiwa kukumbwa na peo la ngono baada ya wanafunzi wake kubainika wakifanya ngono hovyo chooni, madarasani na njiani wakati wa kwenda na kurudi kwenye makazi yao.
Hali hiyo inadaiwa kusababishwa na kushuka kwa kiwango cha elimu shuleni hapo.
Tatizo hilo liliwekwa hadharani jana na Diwani wa Kata ya Nguvumali, Mustafa Seleboss na Mwenyekiti wa Nguvumali Agness Milambo, kwenye bonanza la kampeni za uzinduzi wa kupinga ukatili mashuleni lililoandaliwa na asasi ya kiraia ya Tree of Hope ya jijini Tanga.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao wa Kata ya Nguvumali, walisema asilimia 80 ya wanafunzi wa Sekondari ya Nguvumali wanafanya mapenzi hovyo hata darasani, vyooni na vichakani wakati wakienda au kurudi nyumbani.
Baadhi ya wanafunzi shuleni hapo, Peter Chambai, Hassan Saidy na Teresia John, wamekiri kufanyika kwa vitendo hivyo viovu, ambavyo wameviita ni ukatili na unyanyasaji wa kisaikolojia dhidi ya wanafunzi wasiopenda mchezo huo mchafu.
Wanafunzi hao walisema washiriki wa vitendo hivyo ni wanafunzi kwa wanafunzi au walimu kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tree of Hope, Fortunata Manyeresa, ameahidi kuingia mtaa kwa mtaa kuwasaka wanafunzi wanaojihusisha na vitendo vya ngono wakiwa na umri mdogo ili wanaowarubuni wachukuliwe hatua.
No comments:
Post a Comment