MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday 2 October 2013

MSANII LINNAH SANGA AUNGA MKONO KUHONGWA KWA MTOTO WA KIKE SOMA ZAIDI


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXi-075aMljB0PYy4r-JeMaBGaUO9vNmZKkEZBVaMgsCTRbvF94whyphenhyphenUzdiPxKg9wzSlTE8wmJB7kl1JVhokLMZJvs74LPLaqcEanGGhAAyJTR20wnoZ132tvqwfOf1XiDY9P-Fs9gvwRU/s1600/427384_420273528014665_76005135_n.jpg 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linah Sanga "Ndege Mnana" amewatolea uvivu wale wote wanaozungumza na kuponda kuhusiana na suala la mtoto wa kike kuhongwa na mwanaume.

Linah anasema kwake hana tatizo na yeyote anayehongwa akiwemo yeye mwenyewe kuhongwa akisema ni jambo la kawaida ili mradi liwe na faida.

Anasema yeye mwenyewe binafsi katika kazi zake za ujasiriamali mtaji wake ameupata kwa kuhongwa na mpenzi wake akachanganya na fedha yake na maisha yanakwenda.

Anafafanua kuwa siku zote mpenzi wako hawezi kuacha kukuhonga kwakuwa kwenye mapenzi kusaidiana ni lazima,kwahiyo haoni ajabu yoyote mtu kuhongwa.

"Kusema ukweli mimi mwenyewe boy friend wangu kanisaidia sana na bado anaendelea kunisaidia,mimi sijali mtu aseme lolote analotaka lakini kama nahongwa for benefit sina tatizo na hilo"alisema Linah.

Ameongeza kuwa tatizo watu wamekuwa wana maneno maneno sana na kufuatilia ya watu badala ya kufanya mambo yao lakini ili mradi mambo yake yanakwenda safi hajali lolote anatazama maisha yake zaidi.

No comments:

Post a Comment