MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Monday 21 October 2013

KOCHA WA SIMBA KIBADENI AFUNGUKA NA KUSEMA KAMA SI HUJUMA, NINGEWAFUNGA YANGA ZAIDI YA TATU

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ amesema kwamba kambi yao ya kujiandaa na mchezo wa jana dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga SC ilivamiwa na vijana wakarubuniwa, ndiyo maana timu yake ilicheza ovyo kipindi cha kwanza na kulala 3-0 kabla ya kuzinduka kipindi cha pili na kupata sare ya 3-3.
Akizungumza baada ya mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kibaden alisema kwamba anashukuru kupata sare na anawaheshimu, Yanga kwa kucheza vizuri kipindi cha kwanza na vijana wake kwa kucheza vizuri kipindi cha pili. 
Ningewafunga zidi ya tatu; Kocha wa Simba SC Abdallah Kibadeni kushoto akiwa Msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo kulia.
Hata hivyo, Kibadeni alisema mechi ya jana ilikuwa ashinde yeye zaidi ya mabao matatu, lakini kwa kuwa kipindi cha kwanza wachezaji wake waliwaachia Yanga mabao matatu, wakamvurugia mipango. “Wamewaachia, mimi nasema timu imewaachia wale wamefunga goli tatu. Si timu ya kutufunga goli tatu sisi Yanga namna ile. Lakini waliwaachia. Nikarudi mapumziko nikawaambia sawa, mlitaka kuwaachia tatu, basi zinatosha, mimi niliwaambia hivyo, msiwape nyingi, hizo zinwatosha. Na kweli zimewatosha, tumerudisha goli tatu,”alisema Kibaden na kuongeza; “Wala sijafanya kazi nyingine, nimewaambia tatu mlizowapa wachezaji zinawatosha kwa kutufunga sisi, lakini nyinyi sasa kachezeni mpira,”.   “Nachozungumza, tumepata sare mimi nashukuru. Wenzetu walitangulia kipindi cha kwanza, sisi tukazinduka kipindi cha pili, lakini najua, mimi nimezaliwa Tanzania, mpira wa Tanzania naujua, mpira unachezwa ndani, mpira unachezwa nje,”.
Wachezaji wa Simba SC wakishangilia baada ya kupata sare ya 3-3 wakitoka nyuma kwa 3-0


Simba SC ilikuwa mdondo kipindi cha kwanza


Kipindi cha pili Simba SC walizinduka

“Kuna kazi kubwa sana kuangalia watu wanaovamia kwenye kambi zetu, kwenye timu zetu, kutaka kuharibu kuwadanganya watoto, hawa watoto bado wadogo mimi nasema, sasa hivi wanacheza mpira wa kushinikizwa na watu, ndiyo maana unakuta matatizo tunayoyapata haya,”. “Sasa wengine hawajui, lakini mimi nazungumza kwamba matatizo yapo, timu mliiona kipindi cha kwanza ilifanya vibaya, lakini si kwa kupenda, nimetoka mapumziko nimeongea maneno machache tu nimebadilisha timu, wale wamekuja kucheza mpira sasa, kwa hiyo nataka muwaelimishe watu, wachezaji kucheza mpira ni kazi yao, wawafurahishe wanachama wao, wawafurahishe wapenzi wao,”.  “Sasa wakitumiwa na watu wengine kuja kuvuruga hilo ni tatizo. Sasa kuna vitu mtavisikia baada ya wiki moja au wiki mbili, mimi kila mwenye matatizo natoa, najua mwisho nitapata timu safi, lakini nashukuru matokeo, nawaheshimu Yanga wamecheza mpira mzuri kipindi cha kwanza na mimi nimecheza mpira mzuri kipindi cha pili,”alisema. Akimzungumzia kiungo Abdulhalim Humud aliyeonekana kupwaya jana hadi kutolewa baada ya dakika 45 za kwanza, Kibadeni alisema; “Kuna watu wanamtaka Humud acheze, lakini mimi najua uwezo wa Humud kuna wakati unafikia mahali unakwama, na nimempa nafasi makusudi ili watu waone,”alisema. Simba SC iliingia kwenye mchezo wa jana ikitokea Bamba Beach Kigamboni, Dar es Salaam ambako imekuwa kambi yake tangu wakati wa maandalizi ya msimu, wakati wapinzani wao, Yanga SC walihamia Pemba kwa ki moja kujiandaa na mchezo huo kutoka makao makuu yao, Jangwani. Hadi mapumziko, tayari Yanga walikuwa mbele kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza mawili, lakini kipindi cha Simba SC ikasawazisha kupitia kwa Betram Mombeki, Joseph Owino na Gilbert Kaze. Matokeo hayo yanaifanya Simba SC ibakie nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu kwa kutimiza pointi 19, huku Azam FC ikiendelea kuongoza ligi hiyo kwa pamoja na Mbeya City kwa pointi zao 20 kila timu.
chanzo na bin zubery

No comments:

Post a Comment