MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Sunday 6 October 2013

ADNAN JANUZAJ AGEUKA ALMASI ULAYA ASAKWA KWA UDI NA UVUMBA!

[clip_image001%255B5%255D%255B4%255D.jpg]CHIPUKIZI wa Manchester United Adnan Januzaj, ambae Jumamosi aliipa ushindi Klabu yake katika Mechi yake ya kwanza kabisa kuanza alipopachika Bao zote mbili walipoifunga Sunderland 2-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, sasa anafuatiliwa na England kwa mujibu wa Kocha wa Nchi hiyo Roy Hodgson.

Hodgson amesema: “Ukweli ni kwamba ni Kipaji cha kweli na tunamtazama lakini mambo mengi yanabidi yajadiliwe. Yupo na Man United kwa muda mrefu na inabidi kujadiliana kwa muda mrefu.”
[clip_image001%255B4%255D.jpg] 

Januzaj, mwenye Miaka 18, ambae Asili ya Wazazi wake ni Kosovo lakini Raia wa Albania, kwa sasa anaweza kuzichezea Nchi kadhaa zikiwemo Belgium, Albania na Turkey.

Ili kuichezea England inabidi apate Uraia wa Kujiandikisha au kuhalalishwa baada ya kuishi muda mrefu England.clip_image001[5]Nae Bosi wa Manchester United David Moyes amekiri kuwa FA ya England imewasiliana na Old Trafford kuhusu Januzaj kuichezea England.

Moyes amekiri: “Ndio. Ipo njia ya yeye kuichezea England kupitia yeye kuishi muda mrefu hapa.”
[clip_image002%255B5%255D%255B3%255D.jpg] 

Januzaj ameitwa mara kadhaa kuichezea Belgium lakini amekuwa akikataa huku duru za ndani zikidai mapenzi yake ni kuichezea Nchi ya Asili ya Wazazi wake Albania.clip_image001Januzaj-Wapi katoka:

Mzaliwa wa Belgium Tarehe 5 Februari 1995 kwa Wazazi wenye Asili ya Kosovo na Albanian 1995

Alijiunga na Timu ya Vijana ya Anderlecht Mwaka 2005 na kukaa nayo Miaka 6.  Mwaka 2011, alijiunga na Manchester United.

Akiwa na Timu ya Vijana ya Man United, Januzaj aling’ara sana kiasi ambacho Sir Alex Ferguson alitamka ni  "Ni Mchezaji mzuri mno mwenye uwiano mzuri sana Kisoka!".clip_image002[5]Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu England, alikuwa Benchi kwenye Mechi ya mwisho ya Sir Ferguson walipocheza na WBA kwenye Ligi.

Januzaj alifunga Bao walipocheza huko Hong Kong kwenye ya Kirafiki kabla Msimu kuanza na pia kucheza akitokea Benchi wakati Man United inaifunga 2-0 Wigan kwenye Ngao ya Jamii.

Msimu huu, amecheza Mechi za Ligi, dhidi ya Crystal Palace hapo Septemba 14 na Capital One Cup akitokea Benchi lakini Mechi na Sunderland hapo Jumamosi ndio ya kwanza kuanza.

Januzaj yuko huru kuichezea Belgium au Albania

SOURCE: SOKA IN BONGO

No comments:

Post a Comment