MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Saturday 7 September 2013

WOLPER AWADISI WASANII WANAOVAA NUSU UCHI SOMA ZAIDI

MSANII maarufu wa filamu hapa nchini, Jacqueline Wolper, amewataka wasanii wenzake wa kike kuacha kuvaa nguo zisizo na maadili ya Kitanzania kwa kuwa wao ni kioo cha jamii.

Wolper aliyasema hayo hivi karibuni wakati akihojiwa katika kipindi cha Take One cha Clouds FM, baada ya kuibuka ‘staa’ mwenye muonekano mzuri kuliko wasichana wote katika tasnia hiyo.
Alisema ana imani mashabiki wake wanamkubali licha ya kutovaa nguo zisizokuwa na maadili ya Kitanzania kama wasanii wenzake.
“Mimi nawakubali sana mashabiki wangu kwa kunipigia kura hadi kuibuka mshindi na ni kweli, najiamini kwa kuwa mimi hata siku moja huwezi kuniona nimevaa nguo za nusu uchi kama wengine,” alisema na kuongeza kuwa anajiheshimu na hawezi kuvaa mavazi hayo.
Aliongeza kuwa atajitahidi katika maisha yake aendelee kuvaa mavazi ya heshima, kwani yanampendeza tofauti na wengine ambao wanavaa nguo za nusu uchi na hawapendezi kama yeye.

No comments:

Post a Comment