Huyu
ndiye mhusika mkuu aliyechonga mchongo wote na kumshawishi mwanamke
kutumia kitambulisho chake kufanyiwa wizi huo wa kimtandao.Mrembo akijitetea kuwa hahusiki kabisa katika wizi huu na pia kujitetea kuwa kaacha mtoto mdogo nyumbani.
Hapa akitoa maelezo kuwa yeye si mwizi na hawafahamu kabisa wahusika wenzake na yeye ni mfanyabiashara wa vipodozi.
Mrembo
huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya
kutumia kitambulisho chake na kutaka kuja kurudisha line ambayo siyo
yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika maelezo
yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu Sinza na
wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambayo iliwaleta mpaka
ofisi za Tigo zilizopo Rozana, Buguruni.
Watuhumiwa
wenzake wakificha sura zao huku wakitoa maelezo kwa wafanyakazi wa Tigo
na walinzi waliowatia chini ya ulinzi baada ya kuweka mtego mzuri wa
kuyanasa matapeli hayo ya kimtandao.Kitambulisho
alichotaka kutumia mwanamke kuswap line ambayo sio yake lakini aliweka
jina la mhusika wa line na namba alizokuwa anapiga mara nyingi ndipo
mfanyakazi mmoja wa Tigo kwa jina Octavian Rweyendera alifanikiwa
kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi mara moja.Aliyesimama
hapo yeye alibiwa kiasi cha miioni moja kwa njia ya Sim Banking ya NMB
baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa ali-renew na
kuiba pesa zake.
Hapa mtuhumiwa mmoja akiwa kajilaza chini kwa kugoma kutoa maelezo kwa walinzi.Hapa huyu binti akilia kwa uchungu na kuomba asamehewe.Wakiwa ndani ya gari la polisi kuelekea kituo cha polisi Buguruni.Umati wa watu uliofurika kushuhudia tukio hilo la aina yake.
Mmoja ya wafanyakazi mahiri wa Tigo, Octavian Rweyendera ambaye alifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao akitoa maelezo kwa baadhi ya wa polisi jinsi watuhumiwa walivyotaka kufanya wizi huo wa mtandao.
Askari polisi wakisikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa.
Mmoja ya wafanyakazi mahiri wa Tigo, Octavian Rweyendera ambaye alifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao akitoa maelezo kwa baadhi ya wa polisi jinsi watuhumiwa walivyotaka kufanya wizi huo wa mtandao.
Askari polisi wakisikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa.
(PICHA NA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG)
No comments:
Post a Comment