MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Sunday 29 September 2013

SIMBA WATEMBEZA KICHAPO KWA JKT RUVU, ASHANTI NA AZAM WAKILAZIMISHA SARE

Vinara wa ligi kuu Simba SC wamezidi kujikita kilelen mwa ligi kuu ya vodacom baada ya leo kuwachapa goli 2-0 maafande wa JKT Ruvu katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Simba iliyokuwa na pointi 11 kabla ya mchezo wa leo waliandika goli la kwanza kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Amisi Tabwe katika dakika ya 25.

Penati hiyo ilitokana na mlinzi wa JKT Ruvu kuushika mpira katika eneo la hatari katka harakati ya kuoa hatari langoni mwake, na Amisi Tabwe akapata fursa ya kufunga goli lake la 7 katika michezo mitano aliyocheza.

Simba SC waliandika goli la pili katika dakika ya 50 lililofungwa na RAmadhani Singano 'Messi' aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Amir Kiemba katika kipindi cha kwanza.

Ushindi huo wa leo umewafanya wafikishe point 14 ambapo wametengeza uwazi wa pointi 3 baina yake na na anayemfuata ambaye ni Kagera sugar yenye point 11.
 
Katka uwanja wa Azam Complexs uliopo Chamanzi umeshuhudia Ahanti United waliomaliza pungufu kufuatia kipa wao Amani Simba kuzawadiwa kadi nyekundu wakilazimisha sare ya goli 2-2 na Mtibwa sugar.

Katika mchezo huo Ashanti united walitoka nyuma kwa magoli mawili bila na kurejesha magoli yote na mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.

Wakati katika uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya Prisons wamelazimishwa sare na Azam FC ya goli 1-1, magoli ya kifungwa na Patrick Michael katika dakika ya 36 na lile la Azam FC likifungwa na Kipre Tcheche katika dakika ya 49.

No comments:

Post a Comment