MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Thursday, 22 August 2013

WASHIRIKI WA BONGO STAR SEACH KUKUTANA KAMBINI HIVI KARIBUNI

WASHIRIKI 20 wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search (EBSS), wanatarajia kuingia kambini hivi karibuni jijini Dar es Salaam ili kuanza mafunzo rasmi yatakayofanikisha kupata washiriki bora katika shindano hilo linalotarajiwa kufikia fainali Novemba 17, mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Benchmark Productions Limited, ambao ndio waandaaji wa EBSS, Madam Ritha Poulsen, alisema shindano la mwaka huu linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na jinsi walivyojipanga na kupata washiriki wenye uwezo kutoka mikoani na jijini.

Ritha alisema wameazimia kuingia kambini mapema ili kuwapa fursa washiriki kujifunza zaidi na kuwa na uwezo wa kutosha, ambao utazalisha waimbaji wazuri katika tasnia ya muziki hapa nchini, kupitia kituo cha runinga cha TBC1.

“Mwaka huu washiriki ni wengi, ila tumewapata 20 bora na kutokana na mambo ya kibiashara, kwa sasa EBSS itakuwa inarushwa TBC1 kila Jumapili saa tatu usiku na marudio Jumatano saa 8 mchana, badala ya ITV, kuhama kwetu hakuna ugomvi wala nini ni mambo ya kibiashara, kwani nimeanza kusikia maneno mengine hususan kwenye ‘social media’, sisi hatuko huko, tuko kibiashara zaidi, zaidi ya hapo hakuna,” alisema Ritha.

Naye Balozi wa EBSS, mshindi wa mwaka jana, Walter Chilambo, aliwashukuru vijana kujitokeza kwa wingi katika mikoa mbalimbali ambayo wametembelea, hususan vijana wa kike, ambao walikuwa hawajitokezi kwa wingi.


Naye Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema wao kama wadhamini wakuu wa shindano hilo wamejipanga vya kutosha kuhakikisha linakuwa la aina yake mwaka huu.
Kwa upande wake, Meneja Vipindi wa TBC1, Edna Rajab, aliwahakikisha Watanzania kuwa watahakikisha kipindi cha EBSS kinarushwa kwa ubora wa hali ya juu kila Jumapili na marudio yake Jumatano.
 
 Walter Chilambo na
Mkurugenzi wa Benchmark Productions Limited.
Usaili wa EBSS mwaka huu umefanyika mikoa sita ambayo ni Arusha, Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na Dar es Saalam na sasa usaili unaendelea kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kusailiwa ‘live’, ambapo wanatakiwa wapige simu namba 0901551000 au kutuma ujumbe mfupi kwenda 15530, kama ilivyokuwa kwa mshiriki Meninah Atyk mwaka jana.

No comments:

Post a Comment