Abiria
wapatao 60 waliokuwa wanasafiri na basi la Turu linalofanya safari zake
kati ya mkoa wa Singida na Haidom mkoani Manyara, wamelazimishwa
kuteremka toka ndani ya basi hilo na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 )
wa vijiji vitatu, na kisha kulichoma moto basi hilo.
Taarifa
toka eneo la tukio zinasema wananchi hao ni wa vijiji vya Singa,
Idabagadu na Nkungi mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria
wote wameshuka, walilichoma moto basi hilo ambalo limetekea sehemu
kubwa.
Sababu ya wananchi hao kuchukua uamuzi huo ni kutokana na
basi hilo kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita.
SourceMpekuzi